-
Semina ya kumbukumbu za kufariki dunia Imam Khomeini MA yafanyika Tanzania + Sauti
Jun 02, 2019 23:56Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania Bw. Musa Farhang amesema kuwa Imam Khomeini MA alikuwa mfano wa Mwalimu Nyerere katika misimamo yake ya kulitetea taifa la Palestina n.k. Aidha amewahiiza Waislamu kufuata mambo hayo ili waweze kujikwamua kutoka katika ukoloni wa kifikra. Ammar Dachi na maelezo zaidi kutoka Dar es Salaam...
-
Mmoja auawa, 10 wajeruhiwa kwa risasi za polisi nchini Sudan + Video
Jun 02, 2019 06:58Habari kutoka nchini Sudan zinasema kuwa polisi wa jeshi wamewashambulia kwa risasi wananchi walioendeleza maandamano na kukusanyika mbele ya Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo katika mji mkuu Khartoum na kumuua kijana mmoja wa miaka 20 na kujeruhi wengine 10.
-
Hamas walaani uvamizi wa wanajeshi wa Israel ndani ya Msikiti wa al Aqsa + Video
Jun 02, 2019 06:29Mjumbe mmoja wa ngazi za juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amelaani kitendo cha wanajeshi na walowezi wa Kizayuni cha kuvamia na kuvunjia heshima Msikiti wa al Aqsa na matukufu mengine ya Kiislamu.
-
Kenya yazindua sarafu mpya Madaraka Day + Sauti
Jun 01, 2019 12:23Taifa la kenya limezindua sarafu mpya katika maadhimisho ya 56 ya Madaraka Day ili kupambana na ufisadi. Rais Uhuru Kenyatta amesema kuwa, pasi na kushirikiana ili kuukomesha ufisadi basi ndoto za waanzilishi wa taifa za kuona Kenya ni taifa lililostaarabika katika kila Nyanja, zitashindwa kutimia. Seifullah Murtadha na maelezo zaidi kutoka Mombasa, Kenya.
-
Wananchi wa Tanzania washiriki vikao na maandamano ya Siku ya Quds +SAUTI
May 31, 2019 10:20Mwenyekiti wa Kamati ya Kutetea Haki za Wapalestina nchini Tanzania Abdallah Othman, amemuomba Rais John Pombe Magufuli apaze sauti juu ya suala la kuwaunga mkono Wapelestina, ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakidhulumiwa katika ardhi yao.
-
Waislamu walaumiwa kwa kuuana wenyewe kwa wenyewe na kumsahau adui yao + Sauti
May 27, 2019 11:55Waislamu wa zama hizi wamelaumiwa kwa kumalizana wenyewe kwa wenyewe na kumsahau adui yao halisi. Mwandishi wetu wa Kampala Kigozi Ismail na taarifa kamili.
-
SAUTI, Mahakama Kuu ya Kenya yatupilia mbali pingamizi la mabaradhuli la kutaka kuhalalishwa mahusiano ya jinsia moja
May 24, 2019 11:30Hatimaye Mahakama Kuu nchini Kenya imechukua uamuzi wa kupongezwa, baada ya kukataa kufuta kifungu cha 162 cha sheria za nchi hiyo kinachoharamisha na kupiga marufuku mahusiano ya jinsia moja (yaani ubaradhuli).
-
SAUTI, Rais Mohamed Shein wa Zanzibar akemea upandishaji bei wa bidhaa ndani ya Ramadhan, Chuo cha ndoa ZNZ na Tende zaadimika Kenya
May 24, 2019 10:12Rais Dk Ali Mohamed Shein wa Zanzibar amewakemea wafanyabiashara kupandisha bei kwa bidhaa muhimu zinazotumika sana ndani ya mwezi wa Ramadhan na hata katika miezi mingine. Kadhalika Rais Shein amewaonya wafanya biashara wenye tamaa ya kupata utajiri wa haraka kuacha kuuza biadhaa zilizopitwa na wakati au zile ambazo hazijafikia wakati wa kutumiwa hususan mazao ya shambani.
-
Barua ya Iran kwa Guterres, sisitizo la mazungumzo baina ya nchi za Asia Magharibi + Video
May 22, 2019 22:11Majid Takht-Ravanchi, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa, siku ya Jumanne, Mei 21, 2019 alimwandikia barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na mkuu wa hivi sasa wa Baraza la Usalama la umoja huo kuhusiana na njama za waenezaji fitna wa kigeni kwenye eneo la Ghuba ya Uajemi.
-
SAUTI, Rais John Magufuli Tanzania: Huwezi kupata utajiri wa haraka kwa kupandisha bei bidhaa ndani ya Ramadhani
May 19, 2019 12:54Rais wa John Pombe Magufuli wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania amewataka Watanzania wenye kupandisha bei za bidhaa zinazotumika zaidi ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani waache tabia hiyo mara moja, kama ambavyo pia ametaka kuwepo usimamizi stahiki kuhusiana na suala hilo.