-
Kumbukumbu ya kuuawa shahidi Sheikh Nimr Baqir Al Nimr + Filamu
Jan 02, 2019 04:21Leo Jumatano Januari Pili 2019 ni kumbukumbu ya mwaka wa tatu tokea alipouawa shahidi Sheikh Nimr Baqri al Nimr, mwanazuoni wa Kiislamu na mwanamapambano wa kutetea haki wa Saudi Arabia
-
Iran: Ulaya haina nia ya kweli ya kukabiliana na mashinikizo ya Marekani + Video
Dec 31, 2018 11:43Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Ulaya imeonesha kivitendo kuwa haina nia ya kweli ya kukabiliana na mashinikizo ya Marekani.
-
Zoezi la kuhesabu kura katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo linaendelea + Sauti
Dec 31, 2018 09:59Zoezi la kuhesabu kura linaendelea katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kufuatia Uchaguzi Mkuu uliofanyika jana Jumapili katika nchi hiyo huku wagombea wakuu wa upinzani Felix Tshisekedi na Martin Fayulu wakilalamikia dosari nyingi wanazodai kwamba zilitokea wakati wa kufanyika uchaguzi huo.
-
Jamhuri ya Kiislamu itaendelea daima kuwa pamoja na watu wa Palestina + Video
Dec 30, 2018 03:45"Jamhuri ya Kiislamu itaendelea daima kuwa bega kwa bega na watu wa Palestina na kuyaunga mkono malengo yao matukufu."
-
Kamati ya amani Tanzania inayojumuisha Waislamu na Wakristo yaadhimisha mazazi ya Nabii Isa AS + Sauti
Dec 29, 2018 14:57Kamati ya amani nchini Tanzania ambayo inajumuisha viongozi wa Kiislamu na Kikristo wa madhehebu mbalimbali, imefanya sherehe maalumu za kuadhimisha mazazi ya Nabii Isa AS na mwaka mpya wa Milaadia. Maelezo zaidi yamo kwenye ripoti ya mwandishi wetu Ammar Dachi...
-
Wapinzani kongo DR waendelea kuilalamikia tume ya uchaguzi CENI + Sauti
Dec 27, 2018 23:19Vyama vya upinzani vya Jamhuri ya Kidemokrsia ya Kongo vimeendelea kukosoa hatua ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya nchi hiyo CENI ya kuakhirisha uchaguzi katika miji mitatu nchini humo. Uchaguzi Mkuu wa Rais na Bunge unatarajiwa kufanyika Jumapili hii DRC, lakini hautofanyika katika miji ya Yumbi, Beni na Butembo hadi tarehe 30 Machi mwakani. Mossi Mwasi na maelezo zaidi...
-
Jamii ya kimataifa yahofishwa na uwezekano wa kutokea machafuko wakati wa uchaguzi DRC + Sauti
Dec 24, 2018 23:59Taasisi muhimu za ndani na nje ya Afrika zimeelezea wasiwasi wao kuhusu uwezekano wa kutokea machafuko kabla, wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na zinafikiria njia za kukabiliana na hatari hiyo. Mossi Mwasi na maelezo zaidi...
-
Kuunga mkono Palestina; Sera thabiti ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran + Video
Dec 24, 2018 04:07Ujumbe wa wabunge wa Palestina ukiongozwa na Mahmoud Al Zahar Mkuu wa Mrengo wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, katika bunge, ambaye pia ni mwanachama wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas, uko mjini Tehran kwa lengo la kufanya mazungumzo na wakuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Tanzania yawataka wanahabari kutekeleza vyema majukumu yao + Sauti, Video
Dec 24, 2018 03:31Dk Hassan Abbas, msemaji mkuu wa serikali ya Tanzania amewataka waandishi wa habari nchini humo kutambua haki na kutimiza vyema wajibu wao.
-
Makumi wapoteza maisha katika janga la tsunami nchini Indonesia + Video
Dec 23, 2018 03:50Makumi ya watu wamefariki dunia na wengine wengi kujeruhiwa kutokana na tsunami iliyosababishwa na mripuko wa volcano nchini Indonesia.