Iran yatilia mkazo kusitishwa hatua za mabavu dhidi ya nchi zinazostawi
Mshauri Maalumu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza umuhimu wa kubadilishwa hali na mazingira ya kimataifa kupitia kukomesha hatua za mabavu za upande mmoja dhidi ya nchi zinazostawi duniani.
Nchi wanachama wa kundi la 77 (linaloundwa na nchi 132 zinazostawi duniani) zimebadilishana mawazo kuhusu ushirikiano wa pande mbili na vipaumbele vya kimkakati vya kundi hilo katika mkutano wa kila mwaka wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi Wanachama wa G-77. Mkutano huo umefanyika pambizoni mwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa huko New York Marekani.
Katika mkutano huo, Mohammad Sadegh Fazli Mshauri Maalumu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inatilia maanani suala la kufanyika majadiliano kuhusu mazingira na kufanyika mkutano wa kimataifa wa kupambana na vumbi hapa Tehran.
Wakati huo huo Fadhili amesisitiza kuwa Iran ina azma ya kweli ya kupambana na tatizo hilo kupitia kukuza ushirikiano wa kikanda na kimataifa na kuimarisha maingiliano ya pande kadhaa, umoja na mshikamano kati ya nchi wanachama, kupinga hatua za upande mmoja na maamuzi ya mabavu.
Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama wa kundi la 77 unaofanyika mara moja kila mwaka umefanyika pambizoni mwa mkutano wa Baraza Kuu la UN mjini New York Marekani.