Apr 26, 2024 08:00 UTC
  • Damu ya mashahidi wa hujuma ya kigaidi ya Damascus iliufedhehesha utawala wa Kizayuni

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, damu safi ya mashahidi wa shambulio la kigaidi la utawala wa Kizayuni katika ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus, imeibua heshima na fahari kwa harakati za mapambano ya Kiislamu (muqawama) na kuufedhehsha utawala wa Israel unaotekeleza mauaji ya kimbari.

Rais Ebrahim Raisi wa Jamuri ya Kiislamu ya Iran aliyasema hayo siku ya Alkhamisi alipofika katika nyumba ya shahidi Ali Agha Babaei, mmoja wa mashahidi wa shambulio la kigaidi la utawala wa Kizayuni katika ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus.

Katika kikao hicho ameongeza kuwa: "Mashahidi hawa wanaotekeleza jukumu kubwa la kudumisha usalama wa nchi na wa eneo wmeuawa shahidi na watu makatili zaidi."

Akizungumzia jibu la nguvu la jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa jinai za utawala wa Kizayuni, Raisi amesema: “Hakika athari na baraka za damu ya mashahidi hatimaye zitapelekea kuangamizwa kikamilifu utawala habithi na unatenda jinai wa Israel."

Ikumbukwe kuwa Jumatatu, Aprili 1, 2024, utawala wa Kizayuni wa Israel ulishambulia ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus katika shambulio la kigaidi lililopelekea kuuawa shahidi washauri saba wakuu wa kijeshi wa Iran. Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Iran aliitaja hatua hiyo ya Israel kuwa ni shambulio dhidi ya ardhi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusisitiza kuwa, utawala wa Kizayuni "utaadhibiwa". Katika kutekeleza ahadi hiyo, Jumapili asubuhi (tarehe 14 Aprili 2024), Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu lilichukua hatua ya kuuadhibu utawala huo wa Kizayuni kwa kuvurumisha ndege zisizo na rubani na makombora kuelekea maeneo yanayokaliwa kwa mabavu (Israel) kupitia operesheni ya kuiadhibu Israel iliyopewa jina la Ahadi ya Kweli."