Jun 13, 2024 08:13 UTC
  • Sisitizo la Iran la nchi za Kiislamu kuchukua msimamo imara kwa ajili ya kusimamisha jinai za Israel

Ali Bagheri Kani, Kaimu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran, amesisitiza nchi za Kiislamu kuchukua hatua ya kivitendo kwa ajili ya kukomesha jinai za Wazayuni huko Katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Akizungumza kwa njia ya simu na Hossein Ebrahim Taha, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu, Ali Bagheri Kani amezungumzia kuendelea na kuongezeka jinai za Wazayuni huko katika mji wa Rafah kusini mwa Ukanda wa Gaza, na kutaka kufanyika haraka kikao cha dharura cha mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu kwa ajili ya kuchukuliwa misimamo madhubuti dhidi ya utawala katili wa Israel unaofanya mauaji ya kimbari huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu hasa Ukanda wa Gaza.

Kikao cha jumuiya ya nchi za Kiislamu na Kiarabu mjini Riyadh

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu aidha amelaani jinai hiyo ya Wazayuni na kuzungumzia ulazima wa kuchukuliwa hatua za kivitendo za nchi  za Kiislamu ili kukomesha jinai hizo za utawala haramu wa Kizayuni.

Baada ya miezi minane tangu utawala wa Kizayuni wa Israel uanzishe mashambulizi ya kinyama huko Ukanda wa Gaza, kwa uungwaji mkono kamili wa Marekani na nchi za Magharibi, utawala huo umefanya mauaji makubwa katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan dhidi ya wananchi wasio na ulinzi na madhulumu wa Palestina, ambayo kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni za Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza zaidi ya Wapalestina elfu 37 wameuawa shahidi katika jinai hizo za Wazayuni.

Tags