Sep 26, 2024 03:58 UTC
  • Kamanda: Iran inaona fakhari kumiliki makombora yanayopiga kilomita 2000

Kamanda wa Jeshi la Anga la Iran alisema amesema jeshi la Jamhuri ya Kiislamu linajivunia makombora yenye uwezo wa kupiga shabaha kwa usahihi mkubwa, umbali wa zaidi ya kilomita 2000.

Brigedia Jenerali Qasem Khamooshi amenukuliwa akisema hayo na shirika la habari la Mehr na kuongeza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina kitengo kikubwa na chenye nguvu zaidi cha helikopta katika eneo la Asia Magharibi (Mashariki ya Kati).

Ameeleza kuwa, leo hii, helikopta za Iran zimesheheni zana na vifaa vya kisasa ambavyo vyote vimetengenezwa na wataalamu vijana wa Iran.

Jenerali Khamooshi ameeleza bayana kuwa, “Sasa tuna makombora yenye umbali wa zaidi ya kilomita 2000 na tunailinda nchi kwa umbali mkubwa kutoka kwenye mipaka, na lazima tuendelee na njia hii.” 

Amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo hii imepiga hatua kubwa sana kieneo na kimataifa katika masuala ya ulinzi hasa upande wa nguvu za makombora, na kwamba makombora ya taifa hili yanayopipa kilomita 2000 yanamfanya adui asifikirie hata kuanzisha vita dhidi ya Iran.

Iran imefanikiwa kuzalisha makombora ya kupiga vyombo vya baharini kutokea fukweni, na makombora yote ya Iran kuanzia yale ya kilomita 200 hadi yale ya kilomita 2000 yanapiga shabaha kwa ustadi mkubwa. 

Tags