Rais Pezeshkian kukutana na Marais wa Russia, China na Afrika Kusini
(last modified Wed, 23 Oct 2024 08:03:16 GMT )
Oct 23, 2024 08:03 UTC
  • Rais Pezeshkian kukutana na Marais wa Russia, China na Afrika Kusini

Rais wa Iran, Massoud Bishikian, leo Jumatano atakutana na marais wa Russia, China Afrika Kusini na viongozi baadhi ya nchi zinazoshiriki katika mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Kiuchumi ya BRICS ulianza jana katika mji wa Kazan nchini Russia.

Miongoni mwa masuala yanayojadiliwa katika mkutano huo ni kuimarisha ushirikiano wa pande nyingi kwa ajili ya maendeleo na usalama duniani.

Jioni ya jana Jumanne katika ratiba ya kwanza ya safari yake nchini Russia, Rais Pezeshkian alikutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi na kusema: Uanachama wa Iran na India katika BRICS ni fursa nzuri ya kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili kwa ajili ya kudhamili maslahi ya pande zote. 

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa: Kuimarishwa uhusiano na ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi wanachama kutaboresha kiwango cha ustawi na usalama wa nchi zetu.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi, amesema kuendelea kwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili kunasimama juu ya msingi wa uhusiano wa muda mrefu kati ya staarabu mbili kubwa na mashirikiano ya kitamaduni.

Pezeshkian na Modi

Amesema: Nakubaliana kabisa na wazo la Rais wa Iran la kupanua uhusiano na ushirikiano wa nchi za eneo hili na tunaamini kuwa kuzidisha na kuimarisha uhusiano wa nchi hizi hususan katika uga wa kiuchumi kutadhamini maslahi ya kanda nzima.

Narendra Modi amesema: Mauaji ya watu wasio na hatia huko Gaza na Lebanon hayakubaliki kwa mtazamo wa India na tunashauriana kwa lengo la kurejesha amani na utulivu katika eneo hilo.