Iran na Afrika Kusini zaendeleza mashauriano ili kuimarisha uhusiano
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Afrika Kusini zinaendeleza mashauriano kati yao ili kufuatilia kuimarisha uhusiano wa pande mbili katika nyanja mbalimbali, khususan kisiasa na kiuchumi.
Hussein Jaberi Ansari Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Anayehusika na Masuala ya Nchi za Kiarabu na Afrika leo asubuhi ameelekea Johannesburg Afrika Kusini kushiriki katika Kikao cha Saba cha Kamati ya Pamoja ya kisiasa cha kufuatilia uhusiano kati ya Iran na Afrika Kusini.
Katika ziara yake ya siku mbili nchini Afrika Kusini, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Anayehusika na Masuala ya Kiarabu na Afrika mbali na kushiriki katika kikao hicho kilichotajwa, atakuwa na mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini na Naibu wake. Pande hizo zitajadili kuhusu uhusiano, ushirikiano na masuala mengine yanayozihusu nchi mbili hizo.