Rouhani: Dini na Madhehebu anuwai zimeimarisha umoja wa kitaifa Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i21217
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema uwepo wa dini na madhehebu anuwai hapa nchini umesaidia kuimarisha umoja na mshikamano wa kitaifa.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Dec 11, 2016 14:33 UTC
  • Rouhani: Dini na Madhehebu anuwai zimeimarisha umoja wa kitaifa Iran

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema uwepo wa dini na madhehebu anuwai hapa nchini umesaidia kuimarisha umoja na mshikamano wa kitaifa.

Rais Rouhani ameyasema hayo leo Jumapili kwa mnasaba wa kuingia Wiki ya Umoja wa Kiislamu, alipokutana na maulamaa wa Kisunni hapa Tehran na kufafanua kuwa, uwepo wa dini na madhehebu tofauti haufai kutazamwa kama tishio, bali unafaa kuwa fursa ya kipekee ya kuimarisha umoja wa kitaifa, mshikamano na maendeleo.

Kiongozi wa taifa wa Iran amesema serikali inapania kutumia suala la dini na madhehebu tofauti hapa nchini kuelekea kwenye shina la umoja wa kitaifa na utamaduni. Rais Hassan Rouhani amesema tangu huko nyuma Jamhuri ya Kiislamu imekuwa ikisisitizia suala la kuimarishwa umoja na mshikamano pasina na kuruhusu kugawanywa kwa misingi ya dini na madhehebu.

Wanazuoni wa Kisunni Iran

Kwa upande wao, wanazuoni wa Kisunni hapa nchini wamesema kuna haja ya kuimarishwa umoja kati ya Waislamu wa madhehebu za Shia na Sunni sambamba na kueleza utayarifu wao wa kusaidia kulifikia lengo hilo.

Kadhalika wamelaani jinai za kutisha zinazofanywa na genge la kigaidi na kitakfiri la Daesh katika nchi za Iraq na Syria, nyuma ya pazia la dini.

Mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu Hayati Imam Ruhullah Khomeini alitangaza tarehe 12 Mfunguo Sita Rabiul Awwal hadi tarehe 17 ya mwezi huu kuwa Wiki ya Umoja wa Kiislamu, kwa ajili ya kuimarisha umoja kati ya Waislamu wa madhehebu za Shia na Suni,