Mabaharia wa Iran waachiwa huru Tanzania, wanarejea leo nchini
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, mabaharia wa Kiirani waliokuwa wameingia kikakosa katika maji ya Tanzania na kutiwa nguvuni, wameachiwa huru.
Bahram Qasemi amesema kuwa habari zilizokuwa zimetolewa hapo awali kwamba mabaharia hao wamekamatwa na maharamia wa Somalia si za kweli na kueleza kuwa, waliingia kimakosa katika maji ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amefafanua kuwa, mabaharia hao 8 raia wa Iran waliingia kimakosa katika maji ya Tanzania na kukamatwa na jeshi la nchi hiyo na kwamba kwa sasa wameachiwa huru baada ya ufuatiliaji uliofanyika kuhusu maudhui hiyo.
Ameongeza kuwa mabaharia hao ni wakazi wa mkoa wa Sistan na Baluchestan ulioko kusini mashariki mwa Iran na kwamba, kuna uwezekano kuwa watareje nchini hii leo Jumanne.