Iran: Marekani ichunge mienendo yake katika Ghuba ya Uajemi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i26868-iran_marekani_ichunge_mienendo_yake_katika_ghuba_ya_uajemi
Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Kiislamu limeionya vikali Marekani na kuitaka iwe makini katika harakati zinazofanywa na vikosi vyake vya majini katika Ghuba ya Uajemi.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Mar 26, 2017 03:40 UTC
  • Iran: Marekani ichunge mienendo yake katika Ghuba ya Uajemi

Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Kiislamu limeionya vikali Marekani na kuitaka iwe makini katika harakati zinazofanywa na vikosi vyake vya majini katika Ghuba ya Uajemi.

Naibu Mkuu wa Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Brigedia Jenerali Massoud Jazayeri amepuuzilia mbali madai ya kipropaganda yaliyotolewa hivi karibuni na Washington eti manowari za Iran katika Ghuba ya Uajemi zinaendeleza harakati 'zisizo za kitaalamu na za kichokozi'.

Jazayeri amebainisha kuwa, madai hayo ya Marekani haya na msingi, yamejengeka juu ya taarifa za urongo na yana nia mbaya ya kichokozi.

Lango Bahari la Hormuz

Brigedia Jenerali Massoud Jazayeri amefafanua kuwa, Marekani haina budi kubadilisha mitazamo yake na kuchunga mienendo yake katika Ghuba ya Uajemi.

Matamshi ya Naibu Mkuu wa Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni radiamali kwa tuhuma zilizotolewa na Jeshi la Majini la US, likidai kuwa mnamo Machi 21, ndege ya nchi hiyo iliyokuwa imembeba Rais wa zamani za Marekani, George .W. Bush ilitishiwa na kuchokozwa na meli za kivita za Iran, ilipopaa juu ya Lango Bahari la Hormuz.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa ikiwatahadharisha maadui dhidi ya chokochoko na hatua zozote za kuhujumu mipaka yake ya angani, ardhini na majini.