Ayatullah Amoli Larijani akosoa undumakuwili wa Wamagharibi katika vita dhidi ya ugaidi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i50228-ayatullah_amoli_larijani_akosoa_undumakuwili_wa_wamagharibi_katika_vita_dhidi_ya_ugaidi
Mkuu wa Vyombo vya Mahakama nchini Iran amekosoa vikali undumakuwili wa baadhi ya mataifa ya dunia katika vita dhidi ya ugaidi na kusema kuwa, baadhi ya madola yanadai kupambana na ugaidi na wakati huo huo yanawakingia kifua magaidi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 17, 2018 10:22 UTC
  • Ayatullah Amoli Larijani akosoa undumakuwili wa Wamagharibi katika vita dhidi ya ugaidi

Mkuu wa Vyombo vya Mahakama nchini Iran amekosoa vikali undumakuwili wa baadhi ya mataifa ya dunia katika vita dhidi ya ugaidi na kusema kuwa, baadhi ya madola yanadai kupambana na ugaidi na wakati huo huo yanawakingia kifua magaidi.

Ayatullah Sadeq Amoli Larijani amesema hayo leo katika kikao chake na maafisa wa ngazi za juu wa Idara ya Mahakama ambapo mbali na kuashiria hatua ya Marekani kuanzisha na kuyaunga mkono makundi ya kigaidi kama Daesh amesema wazi kwamba, hatua ya Washington ya kuunda muungano eti wa kukabiliana na ugaidi ni kichekesho na kioja.

Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran ameongeza kuwa, hii leo wananchi wa Iran wanaitwa magaidi katika hali ambayo, katika kipindi cha miaka 40 iliyopita wamekuwa wahanga wa makundi yya kigaidi yanayoungwa mkono na Marekani.

Wanachama wa kuundi la kigaidi la Daesh

Ayatullah Amoli Larijani amesema bayana kwamba, waungaji mkono wa makundi ya kigaidi kama Munafiqeen MKO wamekuwa wakiwakingia kifua watu ambao wamewaua shahidi shakhsia wakubwa wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

Takwimu zinaonyesha kuwa, raia 17,000 wa Iran wameuawa shahidi katika kipindi cha miaka 40 iliyopita kupitia mashambulio ya kigaidi ya makundi ya Muunafiqeen MKO, mtandao wa al-Qaeda, wanagambo wa Taliba  na kkundi la kigaidi na kitakkfiri la Daesh.

Marekani na washirika wake wa Mashariki ya Kati kama Saudi Arabia na Imarati wamekuwa wakiunga mkono na kuyapatia fedha nyingi makundi ya kigaidi ambayo yamekuwa yakiteketeza roho za watu bure bilashi.