Iran yapata mafanikio mapya katika uga wa teknolojia ya nyuklia + Video
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i50845-iran_yapata_mafanikio_mapya_katika_uga_wa_teknolojia_ya_nyuklia_video
Mkuu wa Shirika la Atomiki la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Ali Akbar Salehi amesema nchi yake imeweza kupata mafanikio mapya katika uga wa teknolojia ya nyuklia kwa kuchukua hatua za awali za kutegeneza asilimia 20 ya fueli ya nyuklia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 13, 2019 12:57 UTC
  • Iran yapata mafanikio mapya katika uga wa teknolojia ya nyuklia + Video

Mkuu wa Shirika la Atomiki la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Ali Akbar Salehi amesema nchi yake imeweza kupata mafanikio mapya katika uga wa teknolojia ya nyuklia kwa kuchukua hatua za awali za kutegeneza asilimia 20 ya fueli ya nyuklia.

Akizungumza Jumapili asubuhi, Salehi amesema fueli mpya ya nyuklia ambayo imetayarishwa na wataalamu Wairani ndani ya nchi itaweza kuendesha matanuri nyuklia yote yanayoshabihiana na Tanuri la Nyuklia la Utafiti la Tehran.

Salehi ameongeza kuwa: "hatua za kwaza zimechukuliwa kutegeneza asilimia 20 ya fueli ya nyuklia ya kisasa na mchakato huo unakaribia kumalizika." Amesema bidhaa mpya itakayoundwa ni tafauti na ile ya asilimia 20  ya fueli iliyokuwa ikitumiwa zamani.

 

Mkuu wa Shirika la Atomiki la Iran amesema Tanuri Nyuklia la Utafiti la Tehran limekuwa likitumia fueli ya nyuklia ya zamani na kwamba fueli mpya itaimarisha kiwango cha utendaji kazi.

Salehi amesema wanasayansi Wairani wameweza kupata mafnaikio makubwa katika uga wa teknolojia ya nyuklia na sasa hawana haja tena ya kuiga waliyoyfanya wanasayansi wengine duniani kwani wana uwezo wa kubuni mbinu mpya kama vile kutegeneza fueli mpya na hayo ni mafanikio makubwa kwa Iran. Aidha amesema hivi sasa wataalamu Wairani wanaweza kuunda tanuri nyuklia bila msaada wa kigeni.