Rouhani: Vikwazo dhidi ya Iran havikuwa na faida kwa maadui
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i59192-rouhani_vikwazo_dhidi_ya_iran_havikuwa_na_faida_kwa_maadui
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, vikwazo vilivyowekwa dhidi ya taifa la Iran havina faida kwa maadui na kuongeza kuwa: Jamhuri ya Kiislamu imevuka vikwazo vya kiwango cha juu vya Marekani.
(last modified 2025-10-23T11:19:28+00:00 )
Feb 16, 2020 14:25 UTC
  • Rais Hassan Rouhani
    Rais Hassan Rouhani

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, vikwazo vilivyowekwa dhidi ya taifa la Iran havina faida kwa maadui na kuongeza kuwa: Jamhuri ya Kiislamu imevuka vikwazo vya kiwango cha juu vya Marekani.

Rais Hassan Rouhani ambaye hii leo alikuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Tehran amesema vikwazo vilivyowekwa dhidi ya taifa la Iran havikuzaa matunda yaliyotarajiwa na maadui na kuongeza kuwa, lengo kuu la mashinikizo ya kiwango cha juu ya Marekani dhidi ya serikali na taifa la Iran ni kuburuta Jamhuri ya Kiislamu kwenye meza ya mazungumzo lakini kamwe suala hilo hilo halitatatimia.

Kuhusu mpango wa Amani ya Hormuz, Rais Rouhani amesema: Ni wazi kwa walimwengu wote kwamba, eneo la magharibi mwa Asia haliwezi kupata amani na utulivu bila ya kushirikishwa Iran.

Rais Rouhani

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumzia pia nafasi na mchango wa shahidi Qassem Soleimani aliyekuwa kamanda wa Kikosi cha Quds cha jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika eneo la magharibi mwa Asia na kusema: Shahidi Soleimani alikuwa akifanya juhudi za kuimarisha amani katika eneo nyeti na muhimu la Ghuba ya Uajemi na magharibi mwa Asia. 

Rouhani pia ameashiria mgogoro wa Yemen na kusema: Saudi Arabia inapaswa kukomesha kabisa uvamizi na mshambulizi yake dhidi ya nchi hiyo, na masuala ya Yemene wanapaswa kuachiwa Wayemeni wenyewe.