Zarif: Iran itawatia adabu wachocheao vita
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i60120-zarif_iran_itawatia_adabu_wachocheao_vita
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran amemwambia Rais Donald Trump wa Marekani kwamba Iran haitaanzisha vita lakini itawatia adabu wanaochechea vita.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 02, 2020 04:46 UTC
  • Muhammad Javad Zarif
    Muhammad Javad Zarif

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran amemwambia Rais Donald Trump wa Marekani kwamba Iran haitaanzisha vita lakini itawatia adabu wanaochechea vita.

Muhammad Javad Zarif amejibu madai ya Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya Iran na kuandika katika ujumbe wake uliotolewa leo kupitia ukurasa wa Twitter kwamba: Bwana Trump! Angalia usije ukapotoshwa tena na wanaopenda vita daima, Iran inao marafiki, na hakuna mtu anayeweza kuwa na mamilioni ya "wapiganaji wa niaba".

Dakta Zarif ameongeza kuwa: Tofauti na Marekani inayosema uongo, kughushi na kupotosha, Iran inachukua hatua waziwazi na kwa msingi wa kujihami. 

Muhammad Javad Zarif

Jana Jumatano Rais wa Marekani alidai katika ujumbe wake wa Twitter bila ya kutoa ushahidi wowote kwamba: "Kwa mujibu wa ripoti na uchunguzi, Iran au askari wanaopigana kwa niaba yake wanapanga mipango ya kufanya shambulizi la ghafla dhidi ya askari au maeneo ya Marekani nchini Iraq, iwapo hilo litatokea, Iran italipa gharama kubwa."