Rais Rouhani: Iran sasa hivi inapigana vita vya kulazimishwa vya kiuchumi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i66208-rais_rouhani_iran_sasa_hivi_inapigana_vita_vya_kulazimishwa_vya_kiuchumi
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa sasa hivi Tehran inapigana vita vya kutwishwa vya kiuchumi na kusisitiza kuwa, inabidi taifa na wananchi wla Iran wapongezwe kwa miaka yao 42 ya muqawama, kusimama kidete, subira, kujijenga na kuilinda vizuri nchi yao.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 28, 2021 08:04 UTC
  • Rais Rouhani: Iran sasa hivi inapigana vita vya kulazimishwa vya kiuchumi

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa sasa hivi Tehran inapigana vita vya kutwishwa vya kiuchumi na kusisitiza kuwa, inabidi taifa na wananchi wla Iran wapongezwe kwa miaka yao 42 ya muqawama, kusimama kidete, subira, kujijenga na kuilinda vizuri nchi yao.

Rais Rouhani amesema hayo leo Alkhamisi asubuhi katika sherehe za kuzindua miradi ya taifa ya Wizara ya Jihadi ya Kilimo ya Iran na kuongeza kuwa, inabidi wananchi wa Iran wapongezwe kwa subira na muqawama wao kwenye vita vikubwa na visivyo na mfano katika historia. 

Amesema, katika miaka yote hiyo na hasa kwenye miaka mitatu iliyopita, inabidi tumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwani vita vikubwa kiasi chote hiki vya kiuchumi huenda havijawahi kutokea katika historia ya mwanadamu na ni mara chache mno kuona taifa na nchi kuwekewa mashinikizo kiasi chote hiki katika miongo na karne za hivi karibuni.

Kwa taufiki yake Allah, Iran imeweza kusambaratisha vikwazo vya kibeberu vya Marekani

 

Rais Rouhani amegusia njama za maadui za kutaka kulipigisha magoti na kulivunja nguvu taifa la Iran mbele ya madola ya kiistikbari na kibeberu duniani na kubainisha kuwa, katika kipindi chote hiki cha miaka mitatu taifa letu limesimama imara katika nyuga zote na licha ya kuweko matatizo mengi lakini katika kipindi cha miezi 10 iliyopita Iran imeweza kusafirisha nje bidhaa zenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 28.

Leo ambayo ni Alkhamisi ya 43 ya kaulimbiu ya mapinduzi ya taifa ya uzalishaji wa bidhaa za ndani, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amefungua miradi mitatu mikubwa ya sekta ya kilimo na kulinda rasilimali. Sherehe hizo zimefanyika kwa njia ya video kupitia Intaneti.