Iran: Njia pekee ya kurejesha utulivu katika eneo hili, ni ushirikiano
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i66258-iran_njia_pekee_ya_kurejesha_utulivu_katika_eneo_hili_ni_ushirikiano
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, njia pekee ya kuweza kurejesha utulivu katika eneo hili ni ushirikiano.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 30, 2021 00:56 UTC
  • Iran: Njia pekee ya kurejesha utulivu katika eneo hili, ni ushirikiano

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, njia pekee ya kuweza kurejesha utulivu katika eneo hili ni ushirikiano.

Dk Mohamed Javad Zarif alisema hayo jana katika mtandao wa kijamii wa Twitter na kuongeza kuwa, mazungumzo yake na viongozi wa Uturuki yamekuwa ya kufana. Amesema, katika mazungumzo hayo, pande mbili zimetilia mkazi wajibu wa kuimarishwa uhusiano wa nchi mbili na pia ushirikiano zaidi katika jitihada za kuitafutia ufumbuzi migogoro ya Syria, Iraq na eneo la Caucasia.

Jana Ijumaa, Zarif alionana na Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki mjini Istambul, ikiwa ni kituo cha tano cha safari ya waziri huyo wa mambo ya nje wa Iran katika ziara yake ya kikazi ya mzunguko. 

Bendera za Iran na Uturuki

 

Viongozi hao wawili wamejadiliana masuala muhimu ya pamoja, ya kieneo na ya kimataifa. Kabla ya kuelekea Uturuki, Zarif alitembelea kwanza nchi za Azerbaijan, Armenia, Russia na Georgia.

Siasa kuu za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni mazungumzo baina ya tamaduni tofauti duniani, kutatuliwa matatizo ya dunia kwa njia ya mazungumzo na ushirikiano wa kieneo wa kutatua masuala yaliyopo bila ya kuruhusu madola baki hasa ya kibeberu, kuingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine. Aidha miongoni mwa siasa kuu za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kuwatetea wanyonge popote pale duniani.