Rouhani: Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inatetea wanyonge
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i66308-rouhani_serikali_ya_jamhuri_ya_kiislamu_ya_iran_inatetea_wanyonge
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislmu ya Iran ametoa pongezi zake kwa mnasaba wa kuwadia mwaka wa 42 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kusema: Seikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaunga mkono na kuwatetea wanyonge.
(last modified 2026-03-17T04:36:21+00:00 )
Jan 31, 2021 07:34 UTC
  • Rouhani: Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inatetea wanyonge

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislmu ya Iran ametoa pongezi zake kwa mnasaba wa kuwadia mwaka wa 42 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kusema: Seikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaunga mkono na kuwatetea wanyonge.

Akizungumza leo Jumapili wakati wa kuzindua miradi 13 muhimu ya maji na umeme huko katika mikoa ya Khorasan Kaskazini na Kurdestan, sambamba na kuanza rasmi nchini siku za maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Rais Rouhani amesema: 'Tarehe 12 Bahman (Januari 31) ambayo kinyume na utabiri wa madola ya makubwa, Imam Khomeini (MA) aliweza kurejea nchini na kupokelewa na umati mkubwa wa wananchi usio na mfano wake, ni siku kubwa katika historia ya Iran.'

Dakta Rouhani amesema: Leo ni siku tukufu mno kwa historia na taifa kubwa la Iran, wapenda uhuru na Waislamu wote duniani. Katika siku kama ya leo, Imam Khomeini (MA) aliwasili nchini na kupokelewa na umati mkubwa wa mamilioni ya watu, ambapo kwa kutumia hekima na busara kubwa na kabla ya kufanya jambo jingine lolote alichukua hatua ya kuzuru makaburi ya mashihidi, na hilo ni jambo lenye umuhimu mkubwa.

Kuanza nchini maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu

Akishiria kuzinduliwa miradi muhimu ya kitaifa katika mikao ya Khorasan Kaskazini na Kurdestan katika siku hii muhimu Rais Rouhani amesema: Hata kama mwaka huu umekuwa mgumu kwa wananchi kutokana na vikwazo na janga la corona, lakini uzalishaji mkubwa wa bidhaa nchini ambao Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi aliusisitiza haukuathirika na tokea mwaka huu uanze (wa Kiirani), kila wiki tumekuwa tukifungua miradi muhimu katika kila pembe ya nchi.

Amegusia maendeleo makubwa ambayo yamepatikana katika sekta za maji na umeme na kusema: Baadhi ya watu walikuwa wakidhani kwamba Mapinduzi ya Kiislamu yalikuwa yanahusiana tu na masuala ya kisiasa, kujitawala nchi na mapambano dhidi ya ubeberu na dhulma na wengine wakidhani kwamba yalikuwa yanahusiana tu na umaanawi wa Kiislamu, lakini leo takwimu zinathibitisha wazi kwamba Mapinduzi ya Kiislamu mbali na masuala ya kisiasa na kimaanawi pia yanayapa umuhimu mkubwa masuala ya kimaada.