Vijiji 35,000 Iran vina intaneti ya kasi ya juu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i68158-vijiji_35_000_iran_vina_intaneti_ya_kasi_ya_juu
Iran imefanikiwa kuunganisha intaneti ya kasi ya juu katika maelfu ya vijiji katika kipindi cha miaka minane iliyopita.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 21, 2021 22:01 UTC
  • Vijiji 35,000 Iran vina intaneti ya kasi ya juu

Iran imefanikiwa kuunganisha intaneti ya kasi ya juu katika maelfu ya vijiji katika kipindi cha miaka minane iliyopita.

Kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa Jumapili, idadi ya vijiji vya Iran ambavyo vinapata huduma ya intaneti ya kasi ya juu iliongezeka kutoka takribani sufuri mwaka 2013 hadi vijiji 35,519 kufikia 20 Machi 2021.

Ripoti hiyo imesema vijiji hivyo ni vile vyenye familia zaidi ya 20 na kwamba vijiji vingine 17,000 vinapokea huduma ya intaneti ya kiwango cha wastani.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya Mamlaka ya Mawasiliano ya Iran,  familia milioni 4 katika vijiji 47,000 zimeweza kupata huduma ya simu za mezani na kwamba huduma za posta sasa zinapatikana katika maeneo elfu moja ya mashambani kote Iran.

Huduma za mawasiliano katika kijiji nchini Iran

Aidha taarifa hiyo imesema huduma za intaneti ya kasi nchini Iran zimeimarishwa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita baada ya kuibuka janga la corona ambalo lilisababisha watoto wengi wasomee majumbani kwa kutumia intaneti.