Rabiei: Inabidi vikwazo dhidi ya taifa letu tuvisukumie mbali
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i68160-rabiei_inabidi_vikwazo_dhidi_ya_taifa_letu_tuvisukumie_mbali
Msemaji wa serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, lazima vikwazo vya kidhulma vilivyowekwa na adui dhidi ya taifa letu, tuvipige vita na tuvisukumie mbali.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 21, 2021 22:01 UTC
  • Rabiei: Inabidi vikwazo dhidi ya taifa letu tuvisukumie mbali

Msemaji wa serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, lazima vikwazo vya kidhulma vilivyowekwa na adui dhidi ya taifa letu, tuvipige vita na tuvisukumie mbali.

Ali Rabiei amesema hayo katika mahojiano maalumu aliyofanyiwa na shirika la habari la IRNA na kuongeza kuwa, inabidi vikwazo hivyo tuvirudishe nyuma kikamilifu katika serikali hii hii ya Rais Rouhani ili kulinda heshima na haki za wananchi wetu.

Msemaji huyo wa serikali Rais Hassan Rouhani pia amesema, huko nje pia tumeanza harakati kiasi kwamba katika historia ya kisiasa duniani, Marekani haijawahi kushindwa kiasi hiki ambacho tumeishinda mara hii na haijawahi kutengwa kiasi chote hiki kimataifa kama ilivyotengwa safari hii. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imepata ushindi mkubwa wa kimaadili kimataifa dhidi ya Marekani.

Ali Rabiei pia amezungumzia miundombinu iliyojengwa na serikali ya Iran katika mwaka ulioisha wa 1399 Hijria Shamsia na kuongeza kuwa, kutokana na miundombinu hiyo, tuna matumaini kwamba ugonjwa wa COVID-19 tutaudhibiti kikamilifu mwaka huu wa 1400 Hijria Shamsia.

Licha ya vikwazo vya hali ya juu kabisa dhidi yake, lakini taifa la Iran liko imara. Mwanadamu wa kwanza kufanyiwa majaribio ya chanjo ya corona iliyozalishwa humu nchini

 

Msemaji huyo wa serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amegusia pia miradi mikubwa mikubwa iliyofunguliwa humu nchini na kuongeza kuwa, miradi ya kuzalisha ajira itasukuma mbele maendeleo ya taifa na kuifanya madhubuti mipango ya taifa ya ustawi na maendeleo.

Itakumbukwa kuwa, hivi karibuni, Waziri wa Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu wa Iran alitangaza kuwa chanjo za corona zilizotengenezwa humu nchini zitaanza kutumika katika soko la ndani karibuni hivi. Daktari Saeed Namaki alisema hayo Jumatano na kubainisha kuwa, kuanzia mwezi Ordibehesht 1400 Hijria Shamsia (Aprili 2021) chanjo zilizotengenezwa nchini Iran zitaanza kutumika kwa ajili ya wananchi wote. Waziri wa Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu wa Iran aliongeza kuwa, mashirika ya Iran ya COVIran Barakat, Pasteur, Razi CovPars na Fakhra pamoja na taasisi nyinginezo, yatazalisha chanjo za Kiirani zenye ubora wa hali ya juu, ambazo zitauzwa katika soko la dunia.