Amir Abdullahiyan: Mustakbali wa wananchi haufungamanishwi na nchi yoyote
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i76370-amir_abdullahiyan_mustakbali_wa_wananchi_haufungamanishwi_na_nchi_yoyote
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa mustakbali wa wananchi na nchi yao haufungamanishwi kabisa na mapatano ya JCPOA wala nchi yoyote na kwamba maslahi ya pamoja ndio msingi wa mahusiano.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 31, 2021 04:01 UTC
  • Hussein Amir Abdullahiyan
    Hussein Amir Abdullahiyan

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa mustakbali wa wananchi na nchi yao haufungamanishwi kabisa na mapatano ya JCPOA wala nchi yoyote na kwamba maslahi ya pamoja ndio msingi wa mahusiano.

Hussein Amir Abdullahiyan amesema katika mazungumzo yake na gazeti la Iran kwamba: Tehran imeainisha wazi istilahi kadhaa muhimu kama siasa za nje zenye mlingano na diplomasia hai, imara na erevu katika na kwamba, maana ya siasa hizo za nje zenye mlingano ni kuwa, kutoa kipaumbe kwa baadhi ya nchi zikiwemo nchi jirani hakuna maana ya kupuuza uhusiano wa Tehran na nchi nyingine duniani.  

Ameongeza kuwa, Iran itasogeza mbele diplomasia yenye mlingano katika mahusiano yake na pande zote duniani na kwamba sambamba na serikali ya 13 kutoa kipaumbele kwa nchi jirani na za Asia, Iran pia itatekeleza udiplomasia wenye mlingano, imara na erevu barani Ulaya na haitazisahau nchi za Amerika ya Latini na Afrika. 

Amir Abdullahiyan, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameeleza kuwa, katika upande mwingine Tehran haitaacha kushirikiana na taasisi za kimataifa na inatilia maanani utendaji wa taasisi hizo.   

Ameongeza kuwa, kupitia taasisi hizo za kikanda na kimataifa tunaweza kufuatilia baadhi ya malengo yetu ya sera za kigeni na maslahi ya taifa.