Zarif amjibu Trump: Wazayuni hadi hivi sasa ndio wanaoidhibiti Congress ya Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i76476-zarif_amjibu_trump_wazayuni_hadi_hivi_sasa_ndio_wanaoidhibiti_congress_ya_marekani
Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, amejibu madai mapya ya rais wa zamani wa Marekani Donald Trump aliyedai kuwa, Wazayuni hapo zamani walikuwa wanalidhibiti Baraza la Congress la Marekani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 03, 2021 00:09 UTC
  • Zarif amjibu Trump: Wazayuni hadi hivi sasa ndio wanaoidhibiti Congress ya Marekani

Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, amejibu madai mapya ya rais wa zamani wa Marekani Donald Trump aliyedai kuwa, Wazayuni hapo zamani walikuwa wanalidhibiti Baraza la Congress la Marekani.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Iran Press, Dk Mohammad Jawad Zarif, waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba Trump anadai kwamba Israel ndiyo ambayo hasa iliyokuwa ikiidhibiti Congress ya Marekani, sisi tunasema, hadi hivi sasa bado Wazayuni ndio wadhibiti halisi wa baraza hilo.

Hivi karibuni rais wa zamani wa Marekani Donald Trump alidai katika mahojiano ya redio kwamba kwa takriban miaka 10 Israel ndiyohasa iliyokuwa inaimiliki na Congress ya Marekani na hapo hapo akadai kuwa sasa hivi hali imekuwa kinyume chake. Amedai, hayo ndiyo mabadiliko makubwa aliyoyaona kwenye Congress ya Marekani na kuongeza kuwa. Israel ilikuwa na nguvu kubwa sana ndani ya Congress kwa miaka 15 kwenye kipindi cha zaidi ya miaka 15 iliyopita, lakini sasa hivi inaonekana hali imebadilika.

Donald Trump, rais wa zamani wa Marekani

 

Trump ambaye hafichi chuki na uadui wake dhidi ya wageni na Waislamu hata wenye asili ya Marekani, amegusia pia wabunge wachache waliomo katika bunge la Marekani na kusema kuwa, wabunge hao wanaichukia Israel. Akiwa na nia ya kuchochea zaidi chuki dhidi ya wageni na Waislamu, Trump amesema, wabunge hao wanaichukia kitaasubu Israel. Wabunge hao ndio wanaoidhibi Congress hivi sasa na Israel haina nguvu tena. 

Hata hivyo Dk Mohammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani wa Iran amejibu madai hayo ya Trump na kusema kuwa, mpaka hivi sasa Congress ya Marekani inadhibitiwa na Israel akiashiria jinsi Trump anavyoeneza maneno ya uongo kwa makusudi kwa malengo yake binafsi.