Bagheri Kani: Hitilafu katika mazungumzo ya Vienna zimepungua
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i77968-bagheri_kani_hitilafu_katika_mazungumzo_ya_vienna_zimepungua
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na masuala ya kisiasa amesisitiza kuwa hitilafu zilizokuwepo katika mazungumzo ya Vienna zimepungua.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 13, 2021 01:02 UTC
  • Bagheri Kani: Hitilafu katika mazungumzo ya Vienna zimepungua

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na masuala ya kisiasa amesisitiza kuwa hitilafu zilizokuwepo katika mazungumzo ya Vienna zimepungua.

Ali Bagheri Kani alisema jana kuwa, kuna masuala mawili ya msingi ambayo yanapasa kutenganishwa; suala la kwanza ni hitilafu za kimtazamo kati ya pande husika kuhusu maudhui zinazopaswa kujadiliwa ambapo na suala jingine ni hitilafu za misimamo ya pande mbili kuhusu kadhia zinazojadiliwa.   

Bagheri Kani ameongeza kuwa, hitilafu zilizopo kuhusu maudhui za masuala mbalimbali zimepungua na kwamba pande mbili zinafanya jitihada za kuhitimisha masuala hayo ambayo yanapaswa kuwekwa katika ajenda ya mazungumzo. 

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameeleza pia kuwa, kupungua hitilafu kuhusu maudhui yanayojadiliwa ni hatua nzuri na yenye umuhimu.

Awali Ali Baqeri Kani ambaye anaongoza timu ya Iran katika mazungumzo na kundi la 4+1 alisema katika mazungumzo yake na televisheni ya Press TV kuwa maudhui ambazo ziliibua hitilafu katika duru sita za mazungumzo zilizopita mjini Vienna bado hazijatatuliwa na ziko juu ya meza.

Mazungumzo ya Vienna kati ya Iran na kundi la 4+1 

Amesema Iran haitakubali chochote isipokuwa utekelezaji kamili wa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.