Bagheri Kani: Mazungumzo ya JCPOA huko Vienna ni chanya na yanasonga mbele
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i77994-bagheri_kani_mazungumzo_ya_jcpoa_huko_vienna_ni_chanya_na_yanasonga_mbele
Mkuu wa Timu ya Iran katika mazungumzo na kundi la 4+1 amesema kuwa mazungumzo ya sasa huko Vienna ni chanya na yanaendelea vizuri.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 13, 2021 09:59 UTC
  • Ali Bagheri Kani
    Ali Bagheri Kani

Mkuu wa Timu ya Iran katika mazungumzo na kundi la 4+1 amesema kuwa mazungumzo ya sasa huko Vienna ni chanya na yanaendelea vizuri.

Ali Bagheri Kani amefanya mahojiano na Press TV kuhusu mazungumzo yanayoendelea hivi sasa huko Vienna na kueleza kuwa, Iran imetangaza marekebisho na mapendekezo yake kuhusu masuala inayohitilafiana na pande nyingine husika.

Bagheri Kani ameeleza kuwa, hadi sasa Iran haijapokea pendekezo wala ubunifu wowote kutoka upande wa pili kuhusu masuala wanayohitifiana na kwamba kuna nukta kadhaa kuhusu kadhia mbili za kuondoa vikwazo haramu na vya kidhalimu na pia kuhusu hatua za nyuklia, na kwamba tofauti hizo zinashuhudiwa katika rasimu ya mwisho iliyofikiwa katika duru sita za mazungumzo ya Vienna. 

Mazungumzo ya kuondoa vikwazo dhidi ya Tehran huko Vienna, Austria 

Duru mpya ya mazungumzo ya kuondoa vikwazo vya kidhalimu dhidi ya Iran ilianza huko Vienna Austria siku ya Jumatatu tarehe 29 Novemba. 

Katika duru hiyo ya mazungumzo, timu ya mazungumzo ya Iran  imewasilisha kwa upande wa pili matini ya mapendekezo yake kuhusu kuondoa vikwazo na suala la nyuklia kupitia ubunifu wake mkubwa.