Khatibzadeh: Hatua zimepigwa katika mazungumzo ya Iran na IAEA
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i78054-khatibzadeh_hatua_zimepigwa_katika_mazungumzo_ya_iran_na_iaea
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mapema leo amesema kuwa mafanikio yamepatikana katika mazungumzo kati ya Rafael Grossi, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) na Muhammad Eslami, Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 15, 2021 04:02 UTC
  • Khatibzadeh: Hatua zimepigwa katika mazungumzo ya Iran na IAEA

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mapema leo amesema kuwa mafanikio yamepatikana katika mazungumzo kati ya Rafael Grossi, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) na Muhammad Eslami, Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran.

Saeed Khatibzadeh amesema katika mahojiano yake na Press Tv kwamba, mazungumzo kati ya Eslami na Grossi yamepelekea kupigwa hatua na kupungua mianya kuhusu masuala yaliyokuwa yakiibua hitilafu kati ya pande mbili. Press tv imeripoti kuwa, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa: "Sitaki kuingia ndani zaidi lakini naweza kutabiri kuwa pande mbili karibuni hivi zitafikia mapatano."  

Moja ya mambo yanaibua hitilafu kati ya wakala wa IAEA na Iran ni kuhusu kubadlishwa kamera za uangalizi za wakala huo katika taasisi ya nishati ya atomiki ya Iran huko Karaj ambayo imepata madhara baada ya kukabiliwa na hujuma ya kigaidi. Pande mbili za Iran na IAEA Septemba 12 mwaka huu zilitoa taarifa ya pamoja na kuafikiana  kuhusu huduma zinazopasa kufanywa katika kamera hizo na kubadilishwa kadi za kumbukumbu za vifaa vilivyoainishwa. 

Hata hivyo Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki imeenda mbali zaidi na kutaka kufungwa kamera mpya za ukaguzi; jambo ambalo limepingwa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.