Jan 03, 2022 11:16 UTC
  • Kuuliwa shahidi Qasem Soleiman na kasi ya kuporomoka nafasi ya Marekani eneo la Asia Magharibi

Leo tarehe 3 Januari 2022, inasadifiana na kumbukumbu ya mwaka wa pili wa mauaji ya Jenerali Qasem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu yaliyofanywa na serikali ya Marekani.

Ilikuwa asubuhi ya Januari 3, 2020 wakati habari za kitendo cha jinai cha serikali ya Marekani cha kumuua kigaidi mmoja kati ya makamanda wakuu wa mapambano dhidi ya ugaidi, ilipotangazwa. Serikali ya Marekani ilimuua Jenerali Qasem Soleimani karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad nchini Iraq pamoja na baadhi ya wasaidizi wake, akiwemo Abu Mahdi al-Mohandes, naibu mkuu wa harakati ya wananchi wa Iraq ya al Hashdu al Shaabi. 

Mtazamo wa maadui hususan Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel ulikuwa kwamba, kwa kumuuwa Jenerali Qasem Soleimani aliyekuwa kamanda muhimu zaidi wa muqawama, itawezekana kusimamisha kasi ya kuendelea kupata nguvu kambi ya muqawama ndani ya nchi na katika ngazi ya eneo la Asia Magharibi. Walidhani kwamba, kitendo hicho kiovu kitavuruga mlingano wa nguvu katika eneo hilo la kutoa dhoruba kwa wanamapambano. Hata hivyo, matukio ya miaka miwili iliyopita yamethibitisha kwamba, kwa mara nyingine tena maadui wa kambi ya muqawama na mapambano wana uelewa usio sahihi kuhusu kambi hiyo na imani zake za kidini.

Kuuliwa shahidi Qasem Soleimani kilithibitisha zaidi kwamba moja ya sifa kuu za kambi ya mapambano na muqawama ni upinzani wake mkubwa dhidi ya ubeberu na Uzayuni, ambao unatokana na imani za kidini zisizokubalina na ubeberu na kudhalilishwa na zinawajibisha mapambano dhidi ya madikteta na madhalimu.

Shahidi Qasem Soleimani

Kuuawa shahidi Kamanda Soleimani hakukusimamisha au kudhoofisha mapambano dhidi ya ubeberu na Uzayuni, kinyume chake, siku mbili tu baada ya jinai hiyo ya Marekani, Bunge la Iraq liliidhinisha mpango wa kuwafukuza wanajeshi wa Marekani nchini humo; na tarehe 24 mwezi huo huo wa Januari mamilioni ya Wairaqi walifanya maandamano ambayo yalikuwa hayajawahi kushuhudiwa nchini humo dhidi ya Marekani.  

Aidha, mapigano kati ya makundi ya muqawama na jeshi la Marekani yaliongezeka na kuwa jambo la kila siku nchini Iraq, na serikali ya Marekani ililazimika kuanza duru mpya ya mazungumzo na serikali ya Baghdad kuhusu hali ya wanajeshi wake miezi mitano tu baada ya kuuawa shahidi Jenerali Soleimani, mazungumzo ambayo hatimaye yalipelekea kubadilika hali uwepo wa jeshi la Merekani nchini Iraqi kutoka hali "vita" na kuwa na sifa ya"ushauri".

Hata kama jeshi la Merekani halikuondoka kikamilifu nchini Iraqi kufikia mwisho mwa 2021, lakini kubalishwa hali ya shughuli zake kunamaanisha kuwa, Merekani na wanajeshi wake sio tu kwamba hawawezi kudhamini usalama katika eneo la Asia Magharibi, bali pia ni "tatizo la usalama wa eneo hilo". Sababu kuu ya kukubali mabadiliko hali ya uwepo wa wajeshi wa Marekani nchini Iraq ni wasiwasi juu ya usalama wao na kutaka kupata dhamana ya usalama kutoka kwa serikali ya Iraq.

Hata hivyo, inaonekana kuwa, kama ambavyo Marekani ilikubali kushindwa nchini Afghanistan na kuwaondoa wanajeshi wake kwa madhila nchini humo, hivi karibuni pia italazimika kuwaondoa wanajeshi wake wote nchini Iraq. Kuhusiana na hilo, Faleh Al-Fayadh, mkuu wa harakati ya Al-Hashdu Al-Shaabi, amesema katika hotuba yake ya kuadhimisha mwaka wa pili wa kuuawa shahidi Haj Qasem Soleimani na Abu Mahdi Al-Mohandes, kwamba mauaji ya Soleimani na Al-Mohandes yatakuwa chachu ya kufukuzwa askari wote wa Marekani nchini Iraq.

Hali hii inaashiria kwamba baada ya mauaji ya kigaidi ya Kamanda Soleimani, Asia Magharibi inaelekea kutoka kwenye ramani iliyokuwa imechorwa na Marekani. Haya ni matokeo muhimu na ya kimkakati ya kuuliwa shahidi Kamanda Soleimani, yaliyomfanya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei asisitize kwamba "Shahidi Qasem Soleimani ni hatari zaidi kwa maadui kuliko Kamanda Soleimani."

 

Tags