Iran: Vikwazo ndio chachu kuu ya haki za binadamu za Kimarekani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i89034-iran_vikwazo_ndio_chachu_kuu_ya_haki_za_binadamu_za_kimarekani
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema, kwa miaka mingi wananchi wa Iran wamekuwa wakipapatuana na vikwazo vya kidhalimu vya Marekani na akabainisha kuwa: vikwazo ndio chachu kuu ya haki za binadamu za Kimarekani.
(last modified 2026-08-03T07:36:50+00:00 )
Oct 08, 2022 04:44 UTC
  • Iran: Vikwazo ndio chachu kuu ya haki za binadamu za Kimarekani

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema, kwa miaka mingi wananchi wa Iran wamekuwa wakipapatuana na vikwazo vya kidhalimu vya Marekani na akabainisha kuwa: vikwazo ndio chachu kuu ya haki za binadamu za Kimarekani.

Nasser Kanani Chafi, ameandika katika ukurasa wake wa Instagram kufuatia vikwazo vipya vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Iran ya kwamba: "kila siku na kwa kutumia kisingizio kingine, inatolewa orodha mpya ya vikwazo dhidi ya Iran; na mara hii, Waziri wa Mambo ya Ndani, Waziri wa Mawasiliano na maafisa wengine watano wa Iran wamewekewa vikwazo na serikali ya Marekani".
Kanani Chafi ameongeza kuwa: lakini kabla ya orodha hii ya watu saba ya mawaziri na shakhsia wa Iran, mwananchi mmoja mmoja wa Iran alishaandamwa mara mia kadhaa na vikwazo ambavyo havina mfano wake vilivyowekwa na utawala wa Marekani dhidi ya taifa la Iran katika kila kipindi cha historia.

Tarehe 6 Oktoba, na katika hatua yake mpya ya kuunga mkono machafuko nchini Iran, wizara ya fedha ya Marekani ilitangaza kuwa imeweka majina ya maafisa saba akiwemo Waziri wa Mawasiliano wa Iran katika orodha yake ya vikwazo.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema: Watu wote wa Iran wamekuwa wakitaabika kwa miaka mingi kupambana na vikwazo vya kidhalimu vya Marekani ambavyo vimelenga maisha, ajira, afya na shughuli zao za kawaida bila ya kutenganisha wala kutafautisha yeyote baina yao.
Msemaji wa chombo cha diplomasia cha Iran ameongeza kuwa: Hata watoto wenye maradhi thakili ya ngozi hawakusamehewa na vikwazo vya upande mmoja, visivyo halali na vya kidhalimu vya Marekani; kwani vikwazo ni chachu kuu ya haki za binadamu za Kimarekani.../