Mkutano wa kubainisha harakati za Luteni Jenerali Qassem Soleimani waanza mjini Tehran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i92332-mkutano_wa_kubainisha_harakati_za_luteni_jenerali_qassem_soleimani_waanza_mjini_tehran
Mkutano wa kwanza wa mlolongo wa vikao vya kielimu na kiutafiti wenye shabaha ya kubainisha harakati za Luteni Jenerali Qassem Soleimani chini ya anuani ya "Meza ya Duara ya Kitaalamu ya Vita Dhidi ya Ugaidi na Misimamo ya Kufurutu Ada Asia Magharibi" umeanza leo hapa mjini Tehran.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 31, 2022 04:03 UTC
  • Mkutano wa kubainisha harakati za Luteni Jenerali Qassem Soleimani waanza mjini Tehran

Mkutano wa kwanza wa mlolongo wa vikao vya kielimu na kiutafiti wenye shabaha ya kubainisha harakati za Luteni Jenerali Qassem Soleimani chini ya anuani ya "Meza ya Duara ya Kitaalamu ya Vita Dhidi ya Ugaidi na Misimamo ya Kufurutu Ada Asia Magharibi" umeanza leo hapa mjini Tehran.

Miongoni mwa ajenda za mkutano huo ni kujadili engo ya kimedani, kisheria na kimataifa ya vita dhidi ya ugaidi na mchango wa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani katika kupambana na ugaidi katika eneo la Asia Magharibi.

Miongoni mwa wanaohudhuria mkutano huo ni pamoja na Nasser Kan'ani Chafi, msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamuu ya Iran, Abbas Ali Kadkhodaei, Mkuu wa Kamati Maalumu ya Ufuatiliaji wa Kisheria na Kimataifa wa faili la kuuawa shahidi Qassem Soleimani na Iraj Masjedi, balozi wa zamani wa Jamuri ya Kiislamu ya Iiran nchini Iraq. 

Luteni Jenerali Qasem Soleimani, kamanda wa kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH), ambaye Januari 3, 2020 alikuwa ameelekea Iraq kwa mwaliko rasmi wa viongozi wa nchi hiyo, aliuawa shahidi yeye na Abu Mahdi al-Muhandis, Naibu Mkuu wa jeshi la kujitolea la wananchi wa Iraq la Al Hashdu-Sha'abi pamoja na wanamuqawama wengine wanane usiku wa manane wa kuamkia siku hiyo katika shambulio la anga lililofanywa na jeshi vamizi na la kigaidi la Marekani karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Baghdad nchini Iraq.