161 kugombea viti vya Baraza la Wataalamu Iran
(last modified Wed, 10 Feb 2016 15:22:52 GMT )
Feb 10, 2016 15:22 UTC
  • 161 kugombea viti vya Baraza la Wataalamu Iran

Idara Kuu ya Usimamizi wa uchaguzi wa Iran imesema wagombea 161 wameidhinishwa na Baraza la Walinzi wa Katiba kuwania viti katika uchaguzi wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu Wanaomchagua Kiongozi Muadhamu.

Siamak Rah Peyk, Msemaji wa Idara Kuu ya Usimamizi wa uchaguzi wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu na Baraza la Wanazuoni Wataalamu Wanaomchagua Kiongozi Muadhamu amesema kati ya wagombea 795 waliojiandikisha kugombea viti katika Duru ya Tano la Baraza la Wanazuoni Wataalamu Wanaomcahgua Kiongozi 161 kati yao wameidhinishwa na Baraza la Kulinda Katiba.

Ameongeza kuwa wagombea 220 kati ya wale ambao hawakuidhinishwa waliwasilisha malalamiko yao; na watatu kati yao malalamiko yao yamekubaliwa.

Afisa huyo wa uchaguzi amesema wale ambao wameidhinishwa kugombea uchaguzi katika baraza hilo wanatazamiwa kuanza kampeni zao Februari 11 kwa muda wa siku 14. Uchaguzi wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu utafanyika siku moja na ule wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, Bunge la Iran, tarehe 26 Februari. Baraza la Wanazuoni Wataalamu lina wajumbe 88, nalo Bunge la Iran lina wabunge 290.

Tags