-
Sana’a yalaani uingiliaji wa Marekani katika masuala ya Yemen
Nov 28, 2025 08:12Serikali ya Yemen imelaani vikali hatua ya Marekani ya kuingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo ya Kiarabu na kuitaja kuwa isiyokubalika.
-
Makumi waaga dunia kwa mafuriko Indonesia, Thailand na Malaysia
Nov 28, 2025 08:10Kwa akali watu 250 wamefariki dunia katika mataifa ya Indonesia, Thailand na Malaysia kufuatia mvua kubwa iliyoambatana na mafuriko na maporomoko ya ardhi.
-
Araghchi: Mazungumzo maana yake ni mazungumzo, si ukidteta; Marekani ijirekebishe kwanza
Nov 28, 2025 03:03Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa, Tehran itaendelea kuwa muwazi kuhusu mazungumzo, na msimamo wake utaendelea kuwa ule ule kwamba mazungumzo maana yake ni mazungumzo, si udikteta. Inaweza kufikiria kufanya mazungumzo na Marekani, lakini tu ikiwa Washington itabadilika na kuacha madai yake yasiyo na mantiki. Iingie kwenye mazungumzo ya kuheshimiana na ya usawa si ya kufanyiana udikteta.
-
Afrika Kusini yailaani Marekani kwa kuizuia kushiriki Mkutano wa G20 wa 2026
Nov 28, 2025 03:03Afrika Kusini imelaani nia ya rais wa Marekani Donald Trump ya kuizuia nchi hiyo kuhudhuria Mkutano wa Kundi la 20 (G20) huko Miami, Florida, mwaka ujao.
-
Mwakilishi wa Iran akosoa undumilakuwili wa UN
Nov 28, 2025 03:03Mwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran anayehusika na jamii za wachache amekosoa misimamo ya nyuso mbili na ya kindulimakuwili la Umoja wa Mataifa katika kuyaendea masuala mbalimbali duniani ambayo yanapingwa na madola ya kibeberu.
-
Trump avunja rekodi ya kuwa kiongozi anayechukiza zaidi katika historia ya Marekani
Nov 28, 2025 03:02Marais wa Marekani kwa kawaida huwa wanakumbwa na janga la kupungua umaarufu wa muda mfupi baada ya kuingia madarakani. Lakini kwa mujibu wa The Economist, hakuna rais katika miongo ya hivi karibuni ambaye amepitia janga la kupungua mno umaarufu wake kama lilivyomkuba janga hilo Donald Trump.
-
Putin: Pendekezo la Marekani linaweza kuwa msingi wa makubaliano ya amani ya siku zijazo
Nov 28, 2025 03:02Rais Vladimir Putin wa Russia amesema kuwa, vipengele vya rasimu ya amani vilivyojadiliwa hivi karibuni na Marekani na Ukraine vinaweza kutumika kama msingi wa makubaliano ya siku zijazo ya kukomesha vita nchini Ukraine.
-
Silaha za mauaji ya halaiki na sera za undumilakuwili za Washington na Tel Aviv, chanzo cha migogoro ya kiusalama Magharibi ya Asia
Nov 28, 2025 02:53Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Sayyid Abbas Araghchi amesema, yanayoendelea kujiri katika eneo la Magharibi ya Asia ambayo ni vita vya kudumu, uchokozi wa kivamizi, mauaji ya kimbari na kujipanua kikoloni utawala wa kizayuni wa Israel, ni matokeo ya moja kwa moja ya uungaji mkono wa Marekani na uridhishaji unaofanywa na baadhi ya nchi za Ulaya kwa utawala huo haramu.
-
Kiongozi Muadhamu: Marekani haina hadhi ya kuwa na uhusiano na Iran
Nov 27, 2025 23:30Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema kwenye hotuba yake kupitia televisheni ya taifa kwamba, Marekani haina hadhi ya kuwa na mahusiano na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kwamba vita vya siku 12 vilivyoanzishwa na Marekani na Israel ni vita vilivyopangwa kwa muda wa miaka 20 lakini taifa la Iran limeshinda na adui ameshindwa.
-
Oxfam: Nusu ya Wakenya katika umasikini; matajiri 125 wanamiliki utajiri wa watu milioni 42.6
Nov 27, 2025 23:30Ripoti iliyotolewa na Shirika la Oxfam inaonyesha kuwa, matajiri 125 wanamiliki zaidi ya utajiri wa Wakenya milioni 42.6, huku nusu ya wananchi wakiishi kwa chini ya KSh130 kwa siku.