-
Je, Marekani ni nchi ya demokrasia au Jamhuri ya Mabilionea?
Nov 26, 2025 22:54Ingawa karne moja iliyopita, ni asilimia 0.25 tu ya fedha za uchaguzi wa Marekani ndizo zilizotoka mifukoni mwa watu 100 matajiri zaidi wa nchi hiyo, lakini leo, dola moja kati ya kila dola 13 za chaguzi za serikali ya shirikisho hutoka moja kwa moja kwa mabilionea, jambo ambalo Washington Post imesema kuwa ni kuhodhiwa siasa za Marekani na mabilionea.
-
Uhusiano wa Iran na Pakistan; kiungo cha kimkakati cha amani na utulivu katika eneo
Nov 26, 2025 12:47Ali Larijani, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, amewasili Islamabad na kukutana na kushauriana na maafisa wa Pakistan katika ziara rasmi ya siku mbili.
-
Haaretz: Netanyahu amepelekea Israel kushindwa katika pande zote, hususan dhidi ya Iran
Nov 26, 2025 08:48"Sera za waziri mkuu Benjamin Netanyahu zimepelekea kushindwa Israel katika pande zote za kidiplomasia, kijeshi, na kimkakati, hususan dhidi ya Iran". Hayo ni kwa mujibu wa Haaretz, gazeti la Israel linalochapishwa kwa lugha ya Kiebrania.
-
UNRWA: 90% ya Wapalestina Ghaza wanategemea msaada, wanapitisha siku kwa mlo mmoja
Nov 26, 2025 08:47Shirika la Umoja wa Mataifa la Kutoa Misaada na Ajira kwa Wakimbizi wa Palestina (UNRWA) limesema, hali ya kibinadamu katika Ukanda wa Ghaza ingali ni ya majanga licha ya kusitishwa mapigano, na kuonya kwamba vizuizi vinavyowekwa na utawala wa kizayuni wa Israel kwa uingizaji wa misaada vinaifanya hali ya eneo hilo isiweze kuboreka.
-
Mvutano mkali ulitawala mazungumzo ya Trump na Bin Salman kuhusu kuanzisha uhusiano na Israel
Nov 26, 2025 08:14Duru zenye taarifa zimedokeza kuwa, mkutano kati ya Rais wa Marekani Donald Trump na Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman uliofanyika wiki iliyopita katika Ikulu wa White House ulishuhudia mvutano wa dhahiri kwa sababu Trump aliishinikiza Riyadh ijiunge na Mkataba wa Abraham, wa kuanzisha uhusiano rasmi na utawala wa kizayuni wa Israel.
-
Gavana wa Darfur: Katika kipindi cha siku tatu tu, RSF iliua Wasudan 27,000 El-Fasher
Nov 26, 2025 07:21Gavana wa Jimbo la Darfur nchini Sudan, Minni Arko Minnawi, ameviambia vyombo vya habari kuwa, katika kipindi cha siku tatu tu Wasudan 27,000 waliuliwa na Vikosi vya Usaidizi wa Haraka (RSF) wakati wanamgambo wa vikosi hivyo walipoendeleza wimbi la mauaji baada ya kuuteka mji wa el-Fasher mwishoni mwa mwezi uliopita.
-
Mahakama ya EU yaiamuru nchi mwanachama itambue 'ndoa' za jinsia moja
Nov 26, 2025 07:20Mahakama ya juu zaidi ya Umoja wa Ulaya imetoa hukumu kwamba Poland inalazimika kuzitambua ndoa za jinsia moja zilizosajiliwa katika nchi zingine wanachama wa umoja huo japokuwa mahusiano kama hayo yako kinyume cha sheria kulingana na sheria za kitaifa za nchi hiyo.
-
Asilimia 86 ya vijiji vya Iran vimeunganishwa kwa barabara za lami
Nov 26, 2025 03:44Wizara ya Uchukuzi ya Iran imesema kuwa karibu vijiji tisa kati ya kumi hapa nchini vimeunganishwa kwa barabara za lami; hatua inayoashiria upanuzi mkubwa wa miundombinu ya vijijini nchini Iran.
-
UN: Tangazo la RSF la kusitisha mapigano ni 'hatua katika mwelekeo sahihi'
Nov 26, 2025 03:43Umoja wa Mataifa umekaribisha kwa tahadhari tangazo la kibinadamu la kusitisha mapigano lililotolewa jana na wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF), ukisema kuwa linawakilisha kupiga hatua lakini linahitaji kuidhinishwa kupitia hatua maidanini.
-
Rais wa Nigeria: Wanafunzi wa kike 24 waliotekwa nyara wiki jana wakombolewa
Nov 26, 2025 03:43Wanafunzi wa kike 24 waliokuwa wametekwa nyara kutoka katika shule yao ya bweni wiki iliyopita kaskazini magharibi mwa Nigeria wamekombolewa. Hii ni kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya Rais.