-
Jeshi la Sudan lakabiliana na mashambulizi ya droni katika mji mkuu Khartoum
Nov 08, 2025 00:38Jeshi la Sudan limetangaza kuwa kikosi chake cha ulinzi wa anga jana Ijumaa kilinasa kundi la ndege zisizo na rubani (droni) zilizokusudia kufanya mashambulizi katika mji wa Omdurman, magharibi mwa Khartoum, na katika mji wa kaskazini wa Atbara.
-
Watu 145 washtakiwa kwa uhaini wakidaiwa kuhusika katika maandamano ya vurugu Tanzania
Nov 08, 2025 00:37Waendesha mashtaka nchini Tanzania jana Ijumaa wamewashtaki takriban watu 145 kwa kosa la uhaini madai ya kuhusika katika maandamano ya vurugu yaliyozuka wakati wa uchaguzi wa rais na bunge wiki iliyopita.kulingana na faili za mahakama zilizoonekana na Reuters.
-
Qalibaf: Mataifa ya Kiislamu ‘yanapaswa kutumia nguvu’ dhidi ya Israel
Nov 08, 2025 00:36Mohammad Bagher Qalibaf Spika wa Majlisi ya ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amesema kuwa nchi za Kiislamu "zinapasa kutumia nguvu" dhidi ya utawala wa Israel na kuonya kuwa diplomasia pekee haitazuia vitendo vya uchokozi vya Israel.
-
El Fasher, Hadithi ya Kuanguka Mji
Nov 07, 2025 13:02El Fasher sio jina la mji tu; bali ni jeraha lililowazi la dhamiri ya dunia. Katika kipindi chetu leo, tunasimulia mzingiro uliozuia mkate wa watu, na hujuma iliokata pumzi za watoto. Ni simulizi fupi lakini sahihi, inayotuhimiza sisi sote kuelekeza mazingatio yetu kwa maafa ya binadamu yanayotokea huko Sudan....
-
Je, Gaza itaweza kuepuka mzunguko wa kudumu wa mgogoro bila kufanyika ukarabati wa kimuundo?
Nov 07, 2025 09:02UNICEF kwa mara nyingine tena imetahadharisha kuhusu kuzidi kuwa mbaya mgogoro wa kibinadamu huko Gaza na kusema kuwa zaidi ya watoto milioni moja katika ukanda huo bado wanakabiliwa na ukosefu mkubwa wa maji na chakula, na kuwa wengi hulala njaa kila usiku licha ya kusitishwa mapigano.
-
Rais Pezeshkian: Migawanyiko na mifarakano baina ya Waislamu inaunufaisha Uzayuni wa dunia
Nov 07, 2025 08:22Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, migawanyiko na mifarakano baina ya Waislamu ndilo jambo hasa wanalolitamani maadui wa Uislamu.
-
Kenya yataka majibu kwa Tanzania kuhusu raia wake waliokumbwa na misukosuko ya baada ya uchaguzi
Nov 07, 2025 08:21Kenya imeitaka Tanzania itoe majibu kuhusu hali ya raia wake waliojipata kwenye mzozo wa baada ya uchaguzi, huku ikishinikiza serikali ya nchi hiyo ihakikishe usalama wao na kuchukua hatua dhidi ya ukiukaji wa haki zao.
-
Iran, Mhimili wa Muqawama zalaani ushadidishaji 'hatari' wa mashambulio ya Israel ndani ya Lebanon
Nov 07, 2025 08:06Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani wimbi jipya la uchokozi wa kijeshi unaozidi kufanywa na utawala wa kizayuni wa Israel dhidi ya Lebanon, na kuikumbusha jamii ya kimataifa na nchi za kikanda kuhusu wajibu wao wa kukabiliana na uchochezi wa vita wa Tel Aviv, kwa kuuwajibisha na kuuadhibu utawala huo ghasibu.
-
UN: Israel imekataa maombi zaidi ya 100 ya kuingiza misaada Ghaza tangu vita viliposimamishwa
Nov 07, 2025 06:47Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, tangu yalipoanza kutekelezwa makubaliano ya kusitisha vita tarehe 10 Oktoba, utawala wa kizayuni wa Israel umekataa maombi 107 ya kuingizwa vifaa vya misaada katika Ukanda wa Ghaza, na hivyo kuzuia vifaa muhimu vya kibinadamu kuwafikia Wapalestina wa eneo hilo wanaoishi katika mazingira magumu na ya mateso.
-
Utafiti: Kilimo cha mihadarati ya afyuni nchini Afghanistan kimepungua kwa 20% katika mwaka 2025
Nov 07, 2025 06:47Utafiti mpya uliofanywa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na Madawa ya Kulevya na Uhalifu UNODC umeonyesha kupungua kwa kiasi kikubwa kwa kilimo cha mmea wa afyuni (Opium) nchini Afghanistan katika mwaka huu wa 2025, hali inayoashiria mabadiliko makubwa katika uzalishaji na biashara ya mihadarati katika ukanda huo.