-
Kwa nini Nguvu ya Marekani Inaelekea Ukingoni?
Aug 01, 2026 06:08Miongo mitatu baada ya operesheni ya "Desert Storm," mtazamo ndani ya duru za kimkakati za Marekani ni kwamba zama za nguvu na utawala usio na mpinzani wa Washington zimefikia ukingoni. Vita na Iran vimethibitisha kuwa mwenendo wa mabadiliko katika uwiano wa nguvu na kupungua kwa uwezo wa Marekani wa kuzuia vitisho (deterrence credibility) ndani ya mfumo wa dunia umeanza kushika kasi.
-
Hatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran: Marekani si mchezaji mkuu tena Asia Magharibi
Jul 31, 2026 10:58Imamu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran, amesema Marekani si mchezaji mkuu tena katika eneo la Magharibi mwa Asia, akisisitiza kwamba: "Leo, kwa hatua za Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi na mapambano yanayotokana na maarifa na imani ya wapiganaji wa Jeshi la Iran na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imefikia kiwango cha juu cha kujilinda ambacho kinamfanya adui asiwezi kuanza chochoko ya aina yoyote bila kupata jibu linalofaa."
-
Serikali ya Ghana yaunga mkono kuongezwa muhula wa urais kutoka miaka minne hadi mitano
Jul 31, 2026 10:17Serikali ya Ghana jana Alhamisi ilikubali pendekezo la kuongeza muhula wa urais kutoka miaka minne hadi mitano.
-
Waziri wa zamani Kenya: Rais Ruto anawalazimisha mawaziri kufanya anachotaka kwa woga
Jul 31, 2026 10:04Waziri wa zamani wa Fedha wa Kenya, Prof Njuguna Ndung’u, amemshutumu Rais wa nchi hiyo, William Ruto kwa kuingilia utendakazi wa taasisi huru, akisema mtindo huu umezorotesha uwezo wa kutekeleza majukumu ipasavyo.
-
Droni za Jeshi la Iran zashambulia vituo vya kimkakati vya Marekani nchini Kuwait
Jul 31, 2026 09:59Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limeshambulia vituo vya kimkakati vya jeshi la kigaidi la Marekani katika kambi ya Ahmed al-Jaber huko Kuwait kwa kutumia ndege zisizo na rubani zenye uharibifu mkubwa.
-
Watu kadhaa wafa maji, mamia ya Wamorocco wakimbilia Ceuta ya Uhispania
Jul 31, 2026 08:37Wimbi la wahamiaji kutoka Morocco kuelekea mji unaodhibitiwa na Uhispania wa Ceuta limegeuka kuwa mgogoro wa kibinadamu na kisiasa, baada ya miili ya wahamiaji tisa kuopolewa majini. Wahamiaji hao waliaga dunia wakiwa katika jitihada za kuogelea hadi mjini huo.
-
Baghaei amhoji Guterres; kwa nini unahepa kuwataja wavurugaji wawili wakuu wa sheria za kimataifa?
Jul 31, 2026 03:40Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria matamshi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu kupuuzwa kwa sheria za kimataifa kwa namna inayotisha, na kumhutubu yeye kwa kumwambia: "Sasa ni wakati wa kutimiza jukumu lako zito na kusaidia kuzuia Umoja wa Mataifa na mfumo wa kanuni zake kutofikwa na hatima ya Jumuiya ya Mataifa."
-
Zaidi ya watu milioni 2 wavuka mipaka ya Iran kwa ajili ya Arubaini ya Imam Hussein (AS)
Jul 31, 2026 03:33Zaidi ya mazuwari milioni mbili wa Iran wamevuka salama mipaka ya nchi ili kuhudhuria shughuli ya kila mwaka ya Arubaini ya Imam Hussein, mojawapo ya mikusanyiko mikubwa zaidi ya kidini duniani, inayofanyika katika mji mtakatifu wa Karbala nchini Iraq.
-
Karibu nusu ya Wamarekani wanataka Netanyahu akamatwe licha ya propaganda za mamilioni ya dola
Jul 31, 2026 03:31Karibu nusu ya Wamarekani wanataka waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akamatwe licha ya propaganda zinazofanywa na utawala huo wa kizayuni ambazo zimeugharimu mamilioni ya dola.
-
Al-Nujaba ya Iraq yazionya US na Saudia: Shambulio lenu 'mtalilipia gharama kubwa'
Jul 31, 2026 03:27Harakat ya Hizbullah al-Nujaba ya Iraq imeonya kwamba maslahi ya Marekani na Saudi Arabia "yatalipa gharama kubwa" baada ya mashambulizi ya pamoja ya anga ya nchi hizo kulenga maeneo ya harakati hiyo ya Muqawama katika mikoa kadhaa ya Iraq usiku wa kuamkia jana, na kuua watu wasiopungua 20 na kujeruhi wengine wengi.