Aug 10, 2023 13:28 UTC
  • Kwa mara nyingine walowezi wa Kizayuni wenye chuki na Uislamu wavamia msikiti wa al-Aqswa

Kwa mara nyingine tena walowezi wa Kizayuni wenye misimamo ya kufurutu ada wameuvamia msikiti wa al-Aqswa huko Palestina na kulivunjia heshima eneo hilo takatifu.

Msikiti wa al-Aqsa unajulikana kuwa nembo kuu ya utambulisho wa Kiislamu na Kipalestina wa eneo takatifu la Quds na utawala wa Israel unajaribu kuharibu utambulisho huo, lakini kusimama imara na kuwa macho wananchi wa Palestina kumeufedhehesha utawala huo wa Kizayuni na kupelekea njama zake kushindwa.

Ripoti kutoka Palestina zinasema, walowezi wengi wa Kizayuni wenye misimamo ya kufurutu leo wameuvamia msikiti wa al-Aqswa kibla cha kwanza cha Waislamu na kufanya vitendo vya kichochezi huku wakiwa wanapatiwa ulinzi na vikosi vya usalama vya utawala haramu wa Israel.

Hii si mara ya kwanza kwa walowezi wa Kizayuni kuvamia msikiti wa al-Aqswa wakisaidiwa na wanajeshi wa utawala haramu wa Israel.

Mbali na walowezi wa Kizayuni, askari wa Israel pia wamekuwa wakiuvamia mara kwa mara msikiti wa al-Aqswa

 

Vitendo vya hujuma za walowezi wa Kizayuni dhidi ya msikiti wa al-Aqswa vimekithiri zaidi baada ya kuingia madarakani serikali yenye misimamo mikali ya Benjamin Netanyahu ambayo imekuwa ikionyesha chuki za wazi wazi dhidi ya Wapalestina na maeneo yao matakatifu.

Vitendo vya kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu huko Palestina vinafanyika katika hali ambayo, viongozi wa nchi za Kiarabu na jamii ya kimataifa wameendelea kunyamaza kimya na kutochukua hatua zozote za maana za kukabiliana na vitendo hivyo vinavyokinzana na utu na ubinadamu.

Tags