Sep 22, 2023 11:33 UTC
  • Waziri Mkuu wa Kuwait asisitiza umuhimu wa kadhia ya Palestina

Waziri Mkuu wa Kuwait Ahmad Nawaf Al-Ahmad Al-Sabah amesisitiza kuwa Palestina ni moja ya masuala muhimu katika ulimwengu wa Kiislamu na ulimwengu wa Kiarabu.

Al-Ahmad Al-Sabah amesisitiza hilo katika hotuba yake kwenye mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kueleza kwamba, Palestina inapaswa kuungwa mkono ili iweze kupata haki zake za kimsiingi zilizoghusubiwa.

Kabla ya hapo Rais Mahmoud Abbas wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina alisema katika Mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwamba: "ni ndoto na dhana batili kuweza kuleta suluhu na amani pasi na taifa la Palestina kupata haki zake za kisheria".

Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amesema: "tunaitaka jamii ya kimataifa iwajibike kuhusiana na kuhifadhi hadhi ya kihistoria na kisheria ya Baitul Muqaddas, na tunataka ufanyike mkutano wa kimataifa wa amani utakaohudhuriwa na pande zote zinazohusika na amani katika eneo la Magharibi mwa Asia.

Ahmad Nawaf Al-Ahmad Al-Sabah, Wazirii Mkuu wa Kuwait

 

Vitendo vya hujuma za walowezi wa Kizayuni dhidi ya msikiti wa al-Aqswa vimekithiri zaidi baada ya kuingia madarakani serikali yenye misimamo mikali ya Benjamin Netanyahu ambayo imekuwa ikionyesha chuki za wazi wazi dhidi ya Wapalestina na maeneo yao matakatifu.

Vitendo vya kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu huko Palestina vinafanyika katika hali ambayo, viongozi wa nchi za Kiarabu na jamii ya kimataifa wameendelea kunyamaza kimya na kutochukua hatua zozote za maana za kukabiliana na vitendo hivyo vinavyokinzana na utu na ubinadamu.

Tags