Oct 24, 2023 14:32 UTC
  • Ajuza Muisrael aliyekuwa mateka asimulia alivyokirimiwa na wapiganaji wa HAMAS+VIDEO

Mwanamke mzee Muisrael aliyeachiliwa huru na wapiganaji wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema alikirimiwa na kutendewa wema katika muda wa wiki mbili alipokuwa ameshikiliwa mateka na kundi hilo la wanamapambano wa Palestina.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, Yocheved Lifshitz, ajuza wa miaka 85, amesema Hamas ilimpatia daktari wa kushughulikia afya yake na kufanya kila njia kuhakikisha anapata dawa zake.
 
Ameongeza kuwa wapiganaji wa Hamas walishughulikia pia mahitaji yake. Bi Lifshitz amesema: "tulikula mkate, jibini nyeupe na matango, kama wao."
 
Bi Kizee huyo Muisrael ameendelea kusimulia alivyokirimiwa na wanamuqawama wa Palestina akisema: "walituambia wanaiamini Qur'ani na kwa hivyo hawatatudhuru".
Wanamuqawama wa Brigedi za Izzuddin al Qassam

Alipoulizwa kwa nini alipeana mkono na mmoja wa wanachama wa Hamas wakati wa kuachiliwa kwake, Bi Lifshitz alisema kwa sababu "walliamiliana nasi kwa wema na walishughulikia mahitaji yetu yote."

 
Jumatatu usiku, tawi la kijeshi la Hamas la Brigedi za Al Qassam lilitangaza kuwa limewaachilia huru mateka wawili wa Israel - Yocheved Lifshitz na Nurit Cooper mwenye umri wa 79 - kwa "sababu za ubinadamu."
 
Msemaji wa Al Qassam alisema, kuachiliwa huru wanawake hao wazee kumefanyika kupitia upatanishi wa Qatar na Misri.
 
Tawi hilo la kijeshi la harakati ya Hamas lilieleza hapo awali katika taarifa yake kwamba linawashikilia mateka watu wapatao 200 hadi 250, wakiwemo wanajeshi wa Israel na raia.../

 

Tags