Feb 06, 2024 08:13 UTC
  • Sayyid Hassan Nasrallah
    Sayyid Hassan Nasrallah

Wazayuni wanakiri kwamba, Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrallah, ni kiongozi shupavu na mwenye nguvu zaidi katika Ulimwengu wa Kiarabu na Magharibi mwa Asia.

Kwa mujibu wa gazeti la kikanda la Rai Alyoum, Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon anaendelea kushughulisha vyombo vya habari, na duru za kiusalama na kisiasa za utawala wa Kizayuni wa Israel.

Mchambuzi wa Kizayuni, Yehuda Golkman amemtaja Sayyid Nasrullah kuwa ndiye kiongozi shupavu zaidi katika Ulimwengu wa Kiarabu, ambaye hasiti kutoa changamoto kwa utawala wa Kizayuni wa Israel katika masuala ya vyombo vya habari na ya kijeshi.

Golkman anasema Sayyid Nasrullah ni mtu mzoefu anayeijua Israel vizuri zaidi kuliko adui yeyote mwingine.

Mchambuzi huyo amesema akinukuu duru za usalama, kwamba hadi sasa Hizbullah haijatumia asilimia tano ya uwezo wake na bado ina turufu za kucheza.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, tangu Sayyid Hassan Nasruullah achukue uongozi wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon baada ya kuuawa shahidi Sayyid Abbas Mousawi, mwelekeo wake wote umekuwa katika vita na jeshi la Israel.

Sayyid Hassan Nasrullah

Yehuda Gulkman ameongeza kuwa, Sayyid Hassan Nasrullah anayafahamu vyema matukio ya kisiasa ya sasa ya Israel, hata wasifu wa viongozi wa zamani na wa sasa wa Kizayuni, na tofauti na viongozi wengine wa nchi za Kiarabu, Nasrullah anajulikana kwa ujasiri na ushupavu wake na haogopi makabiliano.

Kwa upande wake, Yisrael Zeif, kamanda wa zamani wa Idara ya Operesheni ya Jeshi la utawala unaofanya mauaji ya kimbari pia ameiambia Kanali 12 ya Televisheni ya Israel kwamba: "Lazima tuwe waangalifu kuhusu Nasrullah, kwa sababu si tu ni kiongozi mwenye nguvu zaidi nchini Lebanon, bali katika eneo zima la Asia Magharibi."

Danny Rubinstein, mchambuzi mwingine wa Israel, pia anasema rais wa zamani wa Misri, Gamal Abdel Nasser alifanya vita kwa siku sita na Israel, lakini Sayyid Hassan Nasrullah aliwalazimisha Waisraeli kukaa kwenye maficho kwa zaidi ya wiki nne katika vita vya 2006.

Tags