Apr 28, 2024 04:27 UTC
  • Amnesty International: Ubaguzi wa apartheid wa Israel dhidi ya Wapalestina hauwezi kukanushwa

Katibu Mkuu wa Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International amesema kuwa, utawala wa Israel umetekeleza ubaguzi wa apartheid dhidi ya Wapalestina. Agnes Callamard amesema kuwa, ameshangazwa mno na utumiaji mabavu wa kimfumo wa utawala ghasibu wa Israel.

Hii ilikuwa ni ziara yangu ya kwanza huko Israel na Palestina; lazima niwaambie kwamba nilishtuka sana wakati wa ziara hii, kwa sababu utumiaji mabavu niliyouona huko haufanani na utyumiaji mabavu mwingine, kwani ulikuwa ni ukandamizaji na dhulma ambayo ya kimfumo na kiuratibu ya utawala wa Israel, amesema katibu mkuu huyo wa Amnesty International.

Wakati huo huo, Wahudumu wa afya, timu za uokoaji na mashirika ya kutetea haki za binadamu yanawashutumu askari vamizi wa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kuwanyofoa viungo Wapalestina na hata kuwazika baadhi yao wakiwa hai kwenye makaburi ya halaiki yaliyogunguliwa kwenye eneo la karibu na Hospitali ya Nasser huko Ukanda wa Ghaza, baada ya askari hao katili kuondoka katika eneo hilo Aprili 7 kufuatia mashambulizi ya ardhini ya miezi minne.

Agnes Callamard, Katibu Mkuu wa Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International

 

Wahudumu wa afya na timu za uokoaji zilizoshiriki katika zoezi la ufukuaji miili ya raia Wapalestina waliozikwa kwenye makaburi ya umati yaliyogunduliwa kwenye eneo la Hospitali ya Nasser huko Khan Younis kusini mwa Ghaza wameripoti kuwa jeshi la Israel limehusika na wizi wa viungo; na kwamba baadhi ya Wapalestina hao walizikwa wakiwa hai kwenye makaburi hayo yaliyogunduliwa hivi majuzi.