Dec 02, 2022 07:54 UTC
  • Bin Salman anaigeuza ardhi ya maeneo matakatifu ya Makka na Madina uwanja wa ufasiki wa kimaadili

Mwandishi wa habari na mpinzani wa utawala wa kifalme wa Saudi Arabia amekosoa kufanyika tamasha la muziki liitwalo MDLBEAST katika ardhi ya maeneo mawili matakatifu (Haramaini-Sharifaini) ya Makka na Madina na kueleza kwamba: Bin Salman anatoa huduma kubwa zaidi kwa maadui wa Uislamu kwa kuigeuza nchi hiyo kuwa uwanja wa kufanyia ufisadi wa kimaadili.

Katika ujumbe alioandika kwenye ukurasa wake wa Twitter, Turki Shalhoub amekosoa kuanzishwa tamasha la muziki liitwalo MDLBEAST ambalo linafanyika kama sehemu ya burudani ziitwazo Msimu wa Riyadh katika mji mkuu huo wa Saudi Arabia, na akasema: "utawala unaoeneza ujahili na upumbavu umechagua kauli mbiu ya 'Tunaidansisha nchi' kwa ajili ya kulitangaza tamasha hili la muziki. Ni nchi gani hiyo wanayotaka kuidansisha? Ni nchi yenye Haram mbili takatifu! Je, kuna uchupaji mkubwa zaidi ya huu wa mipaka ya matakatifu?"

Ujumbe wa Twitter wa Turki Shalhoub

Katika ujumbe wake mwingine wa Twitter Shalhoub ameandika: "ni huduma gani iliyo dhahiri zaidi ambayo bin Salman amewatunukia maadui wa Uislamu? Ameigeuza nchi ya Haramaini kuwa uwanja wa dansi, nyimbo na hafla!"

Tamasha la muziki la MDLBEAST lililoanza jana Alkhamisi Desemba Mosi na kuendelea hadi kesho Jumamosi Desemba Tatu linafanyika kwa kushirikisha waimbaji wa Kiarabu na wa kimataifa katika mji mkuu wa Saudi Arabia, Riyadh.

Bodi ya starehe na burudani ya Saudia inataka kubadilisha utambulisho wa Kiislamu wa jamii ya Saudia kwa kuandaa sherehe na matamasha ya ngoma na miziki katika nchi yenye maeneo mawili matakatifu ya Waislamu ya Makka na Madina licha ya watu wa nchi hiyo kutangaza mara kadhaa wanavyochukizwa na kughadhibishwa kwao na vitendo hivyo vya utawala wa kifalme wa Aal Saud.../

Tags