Feb 01, 2023 07:32 UTC
  • Baraza la Usalama lalaani shambulio la kigaidi lililoua makumi ya watu msikitini Pakistan

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vikali shambulio la kigaidi lililoua makumi ya watu msikitini Pakistan.

Taarifa ya nchi wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa sambamba na kulaani jinai hiyo imetangaza kuwa pamoja na familia zilizopoteza ndugu zao katika tukio hilo la kigaidi na wakati huo huo kuwatakia ahueni haraka majeruhi wa shambulio hilo.

Kabla ya hapo, Umoja wa Mataifa ulikuwa umetoa taarifa na kulaani mlipuko huo wa kigaidi uliotekelezwa katika Msikiti wa Waislamu wa Kishia huko Pakistan. Stephane Dujaric, msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alisema umoja huo unalaani vikali hujuma hiyo ya kigaidi.

Aidha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nayo ilitoa taarifa ya kulaani shambulio hilo sambamba na kusisitiza kulaani kitendo chochote cha kigaidi ambacho kinahatarisha usalama na uthabiti wa nchi na wananchi wa Pakistan.

Kwa upande wake Hizbullah ya L;ebanon sambamba na kulaani jinai hiyo ilieleza kwamba, Taarifa ya harakati hiyo ya muqawama imeeleza kuwa, "Kushupalia makundi ya kitakfiri kutenda jinai za kutisha dhidi ya usalama na uthabiti wa nchi za Kiislamu kunahitaji jibu la ushirikiano wa nchi za Waislamu, ambazo zinapasa kukabiliana na wauaji wanaovaa vazi la dini."

Sikku ya Jumatatu watu wasiopungua 90 waliuawa katika shambulizi la kujilipua kwa bomu lililotokea katika msikiti wa mji wa Peshawar huko kaskazini magharibi mwa Pakistan

Tags