Jun 17, 2024 14:57 UTC
  • Sema uongo na toa vitisho! Baadhi ya maoni ya watumiaji wa X kushambulia propaganda za Israel

Parstoday: Mtumiaji mmoja wa mtandao wa kijamii wa X amesema kuwa Israel na Wazayuni wanapenda sana kutumia mbinu hii ya propaganda kila pale wanapobanwa na jinai zao za kuua raia wa kawaida huko Palestina. Wakibanwa sana utawasikia wanasema, tutafanya uchunguzi. Lakini wakati mashinikizo yanapopungua, vyombo vyao vya habari na wanasiasa wao hujielekeza kwenye jinai nyingine na hakuna uchunguzi wowote unaofanyika.

Leo hii propaganda ni silaha inayotumiwa mno na vyombo vya habari kwa ajili ya kupotosha, kutisha na kuwatia hofu watu. Baadhi ya watumiaji wa mtandao wa kijamii wa X wameandika maoni yao kuhusu propaganda za Israel kuhusu walimwengu na hasa Wapalestina. Baadhi ya maoni hayo ni kama ifuatavyo:

1- Jinsi Marekani inavyoshiriki kwenye propaganda za Israel

S. L. Kanthan, mwanaharakati wa mitandao ya kijamii anagusia namna Marekani inavyoshiriki kwenye propaganda za Israel.

Ameandika:

Kama utatumia sentensi mfano wa "Kuanzia Mto hadi Bahari" au kama utavaa skafu ya Wapalestina basi lazima utaitwa gaidi!

Huu ni moja ya mifano ya propaganda za Israel ambazo zimepenya ndani ya watekelezaji wa sheria nchini Markeani.

Tweet ya Kanthan inayozungumzia jinsi Marekani inavyoshiriki kwenye propaganda za Israel.

 

2- Namna Israel inavyotumia utamaduni kukuza propaganda

Julia ni mwanaharakati mwingine wa mitandao ya kijamii. Ametumia mtandao wa X kugusia ni jinsi gani Israel inavyotumia masuala ya utamaduni kukuza propaganda zake.

Ameandika:

Ninapendekeza kila mtu asome kitabu cha "Paradigm Iliyopotea" kilichoandikwa na mwandishi Myahudi, Jan Lustik. Humo anaonesha moja ya sura za kile anachokiita "Holocastia" na jinsi serikali ya Israel inavyotumia kumbukumbu ya kiutamaduni na kiwewe cha mauaji ya Holocaust kueneza propaganda na kuendesha kampeni dhidi ya Wapalestina.

Tweet ya Julia kuhusu namna Israel inavyotumia vibaya masuala ya utamadunia kueneza propaganda zake.

 

3- Uongo wa Israel kuhusu Intifadha ya Wapalestina

Mtumiaji mwingine wa mtandao wa kijamii wa X anayejulikana kwa jina la El Fares anazungumzia propaganda zilizopitiliza za Israel kuhusu Intifadha ya Palestina:

Ameandika:

Mzee Morgan, hebu twambie...

Je, Intifadha ni kama hivyo zinavyosema propaganda za Israel kwamba wasake kila mahali na ukiwapata Mayahudi waue? Hiyo siyo maana ya neno Intifadha kwa Kiarabu bali maana yake ni mtikisiko, tena linatumika neno hilo wakati Wapalestina wanapoamua kusimama na kuendesha mapambano dhidi ya wavamizi wa ardhi yao. Mfano ni Intifadha ya kwanza iliyofanyika mwaka 1987, ambayo ilitekelezwa kwa amani na Wapalestina lakini Israel iliikandamiza Intifadha hiyo kwa namna ya kinyama kabisa.

Tweet ya Omar El Fares inayozungumizia uongo wa Israel kuhusu Intifadha ya Palestina

 

4- Kufeli mkakati wa propaganda za Israel

Ricardo Damiyan, mwanaharakati mwingine wa mitandao ya kijamii, ametumia mtandao wa X kuzungumzia jinsi stratijia ya propaganda za Israel inavyozidi kufeli na kushindwa.

Ameandika:

Asa Winstanley anasema kuwa, kiwango kikubwa cha maandamano ya kuipinga Israel kinaonyesha kwamba stratijia ya propaganda za utawala ghasibu wa Kizayuni inafeli.

Tweet ya Ricardo kuhusu kushindwa stratijia ya propaganda za utawala wa Kizayuni

 

5- Propaganda za Israel zimeangamiza demokrasia nchini Marekani

Sigma Mindset, mtumiaji mwingine wa mtandao wa kijamii wa X anazungumzia jinsi propaganda za Israel zilivyoangamiza demokrasia nchini Marekani.

Ameandika:

Je, Polisi wa New York hivi sasa wanaendesha propaganda za Israel? Ninapata hisia kuwa, hivi sasa tunashuhudia kuangamia demokrasia.

Tweet ya Sigma Mindset kuhusu sababu za kuangamiza demokrasia nchini Marekani

 

 

6- Uongo wa Wazayuni wa kudai watafanyia uchunguzi uhalifu na jinai zao

Rami G. Khouri, mwandishi wa nchini Marekani anazungumzia uongo mkubwa wa Wazayuni wanapodai kuwa watafanya uchunguzi wa jinai zao.

Ameandika:

Wazayuni wanapenda sana kutumia mbinu hii ya propaganda kila pale wanapobanwa kutokana na jinai zao za kuua raia wa kawaida huko Palestina. Wakibanwa sana utawasikia wanasema, tutafanya uchunguzi. Lakini wakati mashinikizo yanapopungua, vyombo vyao vya habari na wanasiasa wao hujielekeza kwenye jinai nyingine na hakuna uchunguzi wowote unaofanyika.

Tweet ya Rami kuhusu uwongo wa Wazayuni wanapoahidi kufanyia uchunguzi jinai zao

 

7- Furaha ya mrengo wa kulia wa Marekani kutokana na propaganda za Israel

Nuno Marqes ni mchambuzi wa kisiasa ambaye ameulaumu mrengo wa kulia wa Marekani wa kuchekelea kukamatwa wanachuo wa Marekani kutokana na kuiunga mkono kwao Palestina.

Ameandika:

Mrengo wa kulia wa Marekani ni wajinga sana. Wanasherehekea kukamatwa wanachuo wa Marekani kwa propaganda za Israel.

Tweet ya Marqes kuhusu furaha ya mrengo wa kulia wa Marekani kutokana na propaganda za Israel

 

8- Propaganda za uongo za Israel kuhusu kuchomwa moto watoto

Mohamed Osman Ali, Cala, mwanaharakati mwingine wa mitandao ya kijamii naye ametumia mtandao wa X kugusia propaganda za uongo za Israel.

Ameandika:

Propaganda za Israel zimekuja na uzushi wa ngano ya "Watoto wachanga (...) waliowekwa kwenye tanuri na kuchomwa moto wakiwa hai" lakini wakati msichana mmoja wa Djibouti alipodhihaki uigizaji huo wa kitoto wa mauaji ya Holocaust alihukumiwa kifungo kwa madai ya kupinga Uyahudi!

Tweet ya Mohammad Osman kuhusiana na propaganda za uongo za Israel kuhusu kuchomwa moto watoto.

 

9- Wajibu wa kuwa macho mbele ya propaganda za Israel

Mpalestina anayeitwa Ghassan anasisitizia haja ya kuwa macho mbele ya propaganda za Israel.

Ghassan ameandika:

Usikubali kupotoshwa na propaganda za utawala wa Kizayuni. Mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Rafah yanaendelea hivi sasa. Nyumba 11 zimeharibiwa na zaidi ya watu 20 wameuawa katika mashambulizi ya anga ya Israel ya jana usiku.

Tweet ya Ghassan kuhusu wajibu wa kuwa macho mbele ya propaganda za Israel

 

10- Jinsi BBC inavyopigia chapuo na kukariri uongo wa Israel

Simeon Wardle ni mwanaharakati mwingine wa vyombo vya habari. Anazungumzia namna BBC ya Uingereza inavyokariri na kupigia chapuo uongo wa Israel.

Ameandika:

Tangu mwanzo, BBC imekuwa ikikariri na kupigia chapuo uongo wa Israel na hawachungi maadili yoyote ya kusema ukweli wanayotakiwa kuwa nayo waandishi wa habari. Tabaka la wanahabari limetekwa kikamilifu na vyama vya siasa ambavyo navyo vinacheza ngoma inayopigwa na propaganda za Israel. Hawa nao kwa kawaida husaidiwa na wale wanaofaidika na vita.

Tweet ya Simeon Wardle kuhusu namna BBC ya Uingereza inavyopigia chapuo uongo unaoenezwa na Israel

 

11- Propaganda za Israel haziwezi kuficha mauaji ya Wapalestina

Mtumiaji mwingine wa mitandao ya kijamii aitwaye Daddhini anazungumzia jinsi propaganda za Israel zilivyoshindwa kuficha jinai zake dhidi ya Wapalestina.

Ameandika:

Propaganda za Israel haziwezi kuficha ukweli kwamba watu 34,000 wameuawa. Mke, kaka, mtoto wa kiume na binti (wa familia moja). Hind alikuwa na umri wa miaka 6 tu na ameshuhudia familia yake yote ikiuawa mbele ya macho yake. Alistahili kuwa na maisha mazuri lakini kinachoumiza zaidi ni kuiona hadithi ya maisha yake. Maelfu ya watu wengine wameuawa kama yeye.

Tweet ya Daddhini juu ya namna Wazayuni wanavyochuja mno habari

 

12- Marekani na Umoja wa Ulaya bado wamenasa katika propaganda za Israel

Mwanaharakati wa kisiasa anayeitwa Sam anakosoa jinsi Marekani na Umoja wa Ulaya zinavyopuuza jinai na uhalifu wa Israel.

Ameandika:

Inaonekana wazi kwamba wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Columbia (huko Marekani) wanaona mbali zaidi ya propaganda za Israel huku Marekani na Umoja wa Ulaya zikiwa zinahitaji miezi 7 mingine kufahamu kila kitu.

Tweet ya Sam kuhusu Marekani na Umoja wa Ulaya kutekwa na propaganda za Israel na kupuuza jinai za utawala wa Kizayuni

 

Tags