Watu 73 wauawa katika ajali mbaya ya barabarani nchini Afghanistan
https://parstoday.ir/sw/news/uncategorised-i6682-watu_73_wauawa_katika_ajali_mbaya_ya_barabarani_nchini_afghanistan
Kwa akali watu 73 wamepoteza maisha yao na wengine kujeruhiwa vibaya kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea katika mkoa wa Ghazni nchini Afghanistan.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 08, 2016 23:03 UTC
  • Watu 73 wauawa katika ajali mbaya ya barabarani nchini Afghanistan

Kwa akali watu 73 wamepoteza maisha yao na wengine kujeruhiwa vibaya kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea katika mkoa wa Ghazni nchini Afghanistan.

Ajali hiyo iliyotokea jana Jumapili iliyahusisha mabasi mawili ya abiria na lori la mafuta ambapo baada ya kugongana kulitokea mlipuko mkubwa wa moto. Aghagul Jawid Salangi msemaji wa Gavana wa eneo palipotokea ajali hiyo anasema kuwa, ajali hiyo ilitokea katika barabara kuu ya Kabul kuelekea Qandahar yapata kilomita 150 kusini magharibi mwa mji mkuu Kabul.

Taarifa zaidi zinasema kuwa, akthari ya miili ya wahanga wa ajali hiyo imeungua.

Aidha duru za kitiba zinasema kuwa, akthari ya wahanga hao ambao ni wanawake na watoto miili yao imeungua mno na ni vigumu kuweza kuitambua na hali za baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo ni mbaya sana.

Afghanistan imekuwa ikishuhudia ajali za barabarani mara kwa mara ambapo mwezi uliopita watu 18 walipoteza maisha baada ya basi la abiria kupinduka kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

Maafisa wa usalama barabarani wanasema kuwa, ubovu wa barabara na kutoheshimiwa sheria za barabarani ndicho chanzo cha ajali nyingi za barabarni nchini Afghanistan.