Indhari mtawalia kuhusu njama za Marekani na kuhuisha kundi la Daesh
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i101900-indhari_mtawalia_kuhusu_njama_za_marekani_na_kuhuisha_kundi_la_daesh
Katika siku za hivi karibuni, vyanzo vya habari vya ndani nchini Syria na Iraq vimekuwa vikiripoti mara kwa mara kuhusu njama za Marekani za kufufua kundi la kigaidi la Daesh na makundi mengine ya kitakfiri kwa kuwatorosha wafungwa wa kidaesh na kuanzisha uratibu kati ya makundi mengine ya kitakfiri huko Syria.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 05, 2023 23:16 UTC
  • Indhari mtawalia kuhusu njama za Marekani na kuhuisha kundi la Daesh

Katika siku za hivi karibuni, vyanzo vya habari vya ndani nchini Syria na Iraq vimekuwa vikiripoti mara kwa mara kuhusu njama za Marekani za kufufua kundi la kigaidi la Daesh na makundi mengine ya kitakfiri kwa kuwatorosha wafungwa wa kidaesh na kuanzisha uratibu kati ya makundi mengine ya kitakfiri huko Syria.

Kuhusiana na hilo, mwakilishi mmoja wa Syria amesema katika mahojiano na tovuti ya habari ya Al-Ma'luma kwamba, kila mara Marekani inapojikuta iko chini ya mzingiro na kuhisi inashindwa katika medani, hukimbilia katika kuachiliwa huru madaesh kutoka gerezani ili kurejesha mzozo na mvutano nchini Syria.

Chanzo kimoja cha usalama cha Iraq pia kimeiambia tovuti ya habari ya Al-Ma'luma ya kwamba: Kutoroka kwa wafungwa kutoka magereza ya Al-Hasakah na Ghoyran kunapangwa na kuratibiwa na Marekani na kisha kutekelezwa na wanamgambo wa Qasd. Inaelezwa kuwa, waliotoroka kutoka katika magereza hayo ni makamanda wa ngazi za juu wa kundi la kigaidi la Daesh ambao wengi wao walihukumiwa adhabu ya kifo.

Katika siku za hivi karibuni, vyanzo vya habari kaskazini mashariki mwa Syria vimeripoti kutoroka gerezani magaidi wa daesh, tukio ambalo limetokea mara nyingi katika kipindi cha miaka miwili iliyopita na kusababisha kundi hilo la kigaidi kupata uhai na nguvu.

Jenerali Michael Eric Kurilla, kamanda wa Kamandi Kuu ya Marekani, CENTCOM, Agosti 21 alifanya safari nchini Syria na kutembelea kambi kadhaa zilizoko kaskazini mashariki mwa Syria.

Wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh 

 

Kuwepo kwa kamanda huyo wa Centcom katika kambi hizo ambazo ni makazi ya familia za Daesh kulitia nguvu dhana kuhusu njama za Marekani za kulihuisha kundi la kigaidi la Daesh.

Wakati huo huo, "Jabbar al-Maamori" Mwenyekiti wa Umoja wa Wanazuoni wa Kisunni wa Iraq katika mkoa wa Diyala, alionya hivi majuzi dhidi ya njama za Marekani za kutoa mafunzo kwa kizazi cha nne cha Daesh katika kambi ya al-Hawl.

Kambi ya al-Hawl ambayo ina idadi kubwa ya wanachama na familia za kundi la kigaidi la Daesh, iko kaskazini mashariki mwa Syria yapata kilomita 10 kutoka mpaka wa Iraq. Uendeshaji wa kambi hii upo mikononi mwa wanamgambo wa Qasd (vikosi vya kidemokrasia vya Syria) ambao wana mfungamano na Jeshi la Marekani.

Kambi ya Al-Hawl hapo awali ilianzishwa ikiwa na uwezo kuchukua watu 40,000 na ilikuwa na sehemu 6, lakini mnamo 2019, wakati idadi ya watu wa kambi hiyo ilipofikia karibu mara mbili ya uwezo wake, yaani watu 74,000, sehemu mbili zaidi ziliongezwa kwenye kambi hiyo. Hivi sasa, idadi ya watu wa kambi hii inakadiriwa kati ya 50,000 na 60,000, na wakazi wake ni kutoka mataifa 57 tofauti.

 

Weledi wa mambo wanaamini kuwa, moja ya sababu za kuimarika kwa kiasi fulani Daesh katika maeneo ya mashariki mwa Syria na kutekelezwa operesheni za kigaidi katika miezi ya hivi karibuni inahusiana na kutoroka kutoka magereza wanachama wa Daesh. Magereza hayo yapo chini ya udhibiti wa wanamgambo wa Kikurdi na muungano wa Marekani.

Ripoti zinaonyesha kuwa, vikosi vya Marekani vimeanzisha kambi za mafunzo kwa makundi ya kigaidi yenye mafungamano na Daesh mashariki mwa Furat nchini Syria, hususan Bukamal na Deir ez-Zor.

Hofu ya muungano wa kiuchumi wa Iran, Iraq, Syria na Lebanon, kupunguzwa athari za vikwazo na muhimu zaidi kubadilishwa kwa maeneo yenye migogoro kuwa barabara kuu za kiuchumi, ni miongoni mwa mambo ambayo yameilazimu Marekani kuvuruga kivuko cha Bukamal.

Marekani ilirejesha vikosi vyake vya kijeshi nchini Iraq mwaka 2014 kwa kisingizio cha kupambana na kundi la Daesh, na kufuatia kupanuka kwa uwepo wa kundi hilo la kigaidi kutoka Iraq hadi Syria, Washington nayo ilipanua pia uwepo wake katika maeneo ya ardhi ya Syria, haswa katika maeneo yenye utajiri wa mafuta. Filihali kuna kambi 28 za kijeshi za Marekani nchini Syria ambazo ni mjumuiko wa kambi 24 za kijeshi na kambi 4 za vifaa vya kilojistiki ambazo zina takribani wanajeshi 2,000.

Msafara wa jeshi la Marekanii nchini Syria

 

Wajuzi wa mambo wanaamini kuwa, endapo kundi la Daesh litahuishwa na Marekani kwa njia yoyote ile, basi hapana shaka kuwa, Umoja wa Ulaya na nchi wanachama wa umoja huo wa kisiasa na kiuchumi ndio watakaokuwa waaathiriwa wakuu. Licha ya kuwa, mkakati wa kuhuisha Daesh na makundi mengine ya kitakfiri nchini Syria hata kama hilo linafanyika kwa maslahi ya Marekani kwa ajili ya kuwapotosha walimwengu kuhusiana na vita vya Russia na Ukraine au kwa maslahi ya utawala haramu wa Israel kwa ajili ya kukata mawasiliano ya mhimili wa muqawama, lakini bila shaka utakaodhurika ni Umoja wa Ulaya.

Hii ni kutokana na kuwa, idadi kubwa ya wanachama wa Daesh walioko katika kambi ya al-Hawl ni raia wa Ulaya. Licha ya kuwa hadi sasa mataifa ya Ulaya yametia ngumu kuwapokea magaidi hao, lakini kama mwenendo wa kuwatorosha wanachama wa kundi la kigaidi la Daesh kutoka katika magereza huko katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu Syria na Iraq utaendelea, na hivyo kizazi cha nne cha Daesh kikatoka katika kambi ya al-Hawl na kuingia uwanjani, ni jambo lisilo na shaka kwamba, kwa haraka au kwa kuchelewa wataingia barani Ulaya   na hivyo kuzisababishia matatizo nchi hizo