Holocaust Halisi Inafanyika Ukanda wa Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i103672-holocaust_halisi_inafanyika_ukanda_wa_gaza
Juzi usiku utawala wa Kizayuni wa Israel ulifanya jinai isiyo na kifani kwa kushambulia Hospitali ya al-Ma'madani katika Ukanda wa Gaza kwa bomu lenye uzito wa tani moja na kuua shahidi raia karibu elfu moja na mia moja.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 19, 2023 04:08 UTC
  • Holocaust Halisi Inafanyika Ukanda wa Gaza

Juzi usiku utawala wa Kizayuni wa Israel ulifanya jinai isiyo na kifani kwa kushambulia Hospitali ya al-Ma'madani katika Ukanda wa Gaza kwa bomu lenye uzito wa tani moja na kuua shahidi raia karibu elfu moja na mia moja.

Mamia ya raia wengine wa Palestina walijeruhiwa, wengi wao wakiwa ni watoto na wanawake.

Jinai hiyo iliyofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel imetajwa kuwa ndio holocaust halisi. Ni kielelezo halisi cha mauaji ya kimbari. Jarida la Kimarekani la Wall Street Journal limetangaza kuwa: Bomu lililotumiwa kushambulia Hospitali ya al-Ma'madani huko Gaza ni la Kimarekani aina ya MK-84, ambalo lina uzito wa takriban tani moja na lina nguvu kubwa sana ya uharibifu.

Gaza

Utumiaji wa bomu hilo la Marekani lenye uzito wa tani moja umeifanya idadi ya wahanga wa Hospitali ya Ma’madani kuwa kubwa mara nne zaidi ya uhalifu na jinai ya Deir Yassin, mwaka 1948.

Hapa kuna nukta kadhaa muhimu kuhusu jinai ya Wazayuni katika shambulio la bomu kwenye Hospitali ya Al-M'amadani huko Gaza:

Utawala wa Kizayuni wa Israel uliishambulia kwa bomu hospitali hiyo wakati ukijua kuwa, kulikuwa na wagonjwa na majeruhi wengi ndani ya hospitali hiyo. Utawala wa Kizayuni ulilenga kwa makusudi hospitali hiyo ili kufidia kushindwa na kipigo cha aina yake katika operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa; hata hiyo jinai ya Al-Ma’madani imedhihirisha tena sura ya kinyama na ya kigaidi ya utawala wa Kizayuni mbele ya macho ya walimwengu.

Vilevile jinai ya Al-Ma’madani imethibitisha kushindwa mbinu za kidhalimu za utawala unaoikalia Quds kwa mabavu na kwa mara nyingine imeonyesha kuwa utawala huo ndio utawala khabithi na mtenda jinai mkubwa zaidi katika upeo wa dunia nzima. Picha za maiti zilizokatwa vipade vipande za wahanga wa uhalifu huo, hususan watoto wadogo, zinaonyesha kuwa kimsingi haki za binadamu hazina maana yoyote kwa nchi za Magharibi. Uhalifu huu ulifanyika wakati Kansela wa Ujerumani, Olaf Scholz, alikuwa mjini Tel Aviv, na kabla kidogo ya ziara ya Rais wa Marekani, Joe Biden katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Kwa maneno mengine ni kuwa, jinai hiyo ya Wazayuni imetekelezwa kwa himaya na uungaji mkono kamili wa nchi za Wamagharibi.

Kwa mtazamo wa Magharibi, vita, kama ulivyo ugaidi, vinagawanywa katika vita vizuri na vibaya. Vita vya Russia dhidi ya Ukraine vinatambuliwa na Wamagharibi kuwa ni vita vibaya, lakini vita na mauaji yanayofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya watu wa Gaza ni jambo zuri na la kuungwa mkono! Hii ndio mantiki ya haki za binadamu ya nchi za Magharibi. Tumeshuhudia kwamba, Marekani, Uingereza na Ufaransa zimekwenda mbali katika kuukingia kifua utawala haramu wa Israel kwa kupiga veto muswada uliopendekezwa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kusitisha vita na sio kuilaani Israeli.

Nchi za Kiislamu ndizo wahasiri wakubwa wa vita na uhalifu huu ikiwa hazitachukua hatua kali na madhubuti dhidi ya jinai ya Hospitali ya Al Ma’madani. Mataifa ya Kiislamu yamekasirika na maandamano ya kuunga mkono Palestina yanaendelea kufanyika katika nchi nyingi za Kiislamu.

Watu katika nchi mbalimbali duniani na hata katika miji mashuhuri ya Ulaya na Marekani wanaendelea kufanya maandamano makubwa wakipinga jinai na uhalifu unaoendelea kufanywa na Israel ikiungwa mkono na Marekani na washirika wake wa Ulaya. Huko Jordan wananchi wameuchoma moto ubalozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel mjini Amman. Nchini Qatar, maandamano ya kupinga Marekani na Israel yamefanyika mbele ya ubalozi wa Marekani kulaani shambulio la bomu katika Hospitali ya Al-Ma'madani huko Gaza, na yalikuwa maandamano ya kipekee na ya aina yake, kwa sababu hadi sasa hakujawahi kushuhudiwa maandamano kama hayo ya wananchi mbele ya Ubalozi wa Marekani nchini Qatar.