Idadi ya wahanga wa miripuko ya kigaidi Baghdad yaongezeka
(last modified Sun, 03 Jul 2016 13:36:39 GMT )
Jul 03, 2016 13:36 UTC
  • miripuko ya kigaidi Baghdad
    miripuko ya kigaidi Baghdad

Duru za habari zimeripoti kuwa idadi ya wahanga wa miripuko ya kigaidi iliyotokea Baghdad mji mkuu wa Iraq imeongezeka na kufikia watu 165.

Idadi ya wahanga wa mripuko wa kwanza uliotokea baada ya gari lililokuwa limetegwa bomu ndani yake kuripuka karibu na Husseiniya ya Abdulrasul katika wilaya ya al Karrada katikati mwa Baghdad na mlipuko mwingine wa bomu uliotokea karibu na soko la Shalal katika eneo la al Sha'ab kaskazini mwa Baghdad imefikia watu 165 na majeruhi 168.

Kabla ya hapo duru za habari zilitaja idadi ya watu waliouliwa kwenye miripuko hiyo ya kigaidi huko Baghad kuwa 86 na wengine karibu ya 200 kujeruhiwa.

Kundi la kigaidi la Daesh limetangaza kuhusika na miripuko hiyo ya Baghdad. Wakati huo huo Taasisi ya Kupambana na Ugaidi ya Iraq imetangaza kuwa imemtambua na kumtia mbaroni kibaraka mmoja wa kundi la kigaidi lilihusika na mripuko wa kigaidi katika wilaya ya al Karrada.