Feb 12, 2016 08:16 UTC
  • Arubaini ya Sheikh Nimr yaadhimishwa kwa maandamano

Arubaini ya Sheikh Nimr Baqir al-Nimr, mwanachuoni wa Kiislamu aliyeuawa shahidi na utawala wa Aal-Saud imeadhimishwa kwa maandamano ya maelfu ya watu nchini Saudi Arabia na Bahrain.

Huko Saudia, maandamano hayo yamefanywa katika mkoa wa mashariki wa Qatif, ambapo waandamanaji walikuwa wakipiga nara za "Mauti kwa Aal-Saud" wakilaani mauaji ya kikatili ya msomi na mwanaharakati huyo wa Kiislamu. Baadhi ya mabango yaliyokuwa yamebebwa na waandamanaji hao yalikuwa na ujumbe unaosema kuwa "Mikono ya serikali ya Riyadh imejaa damu ya watu wasio na hatia". Maandamano hayo yamefanyika siku moja baada ya familia ya Sheikh Nimr kuutaka ukoo wa Aal-Saud kuikabidhi mwili wa mpendwa wao ili iusitiri. Utawala wa Aal Saud tarehe Pili Januari mwaka huu ulimnyonga msomi huyo mkubwa wa Kishia, hatua iliyokabiliwa na wimbi kubwa la malalamiko kutoka nchi mbalimbali hususan katika ulimwengu wa Kiislamu. Muhammad Nimr, mwana wa kiume wa msomi huyo hivi karibuni alinukuliwa akisema kuwa, utawala wa Aal Saud unafanya njama mbalimbali kuzusha fitna na migawanyiko kati ya Waislamu wa Kishia na Kisuni katika eneo hili na kuongeza kuwa watawala wa Saudia walimnyonga baba yake kutokana na misimamo yake ya kutetea haki za raia wa nchi hiyo, kinyume na madai yanayotolewa na baadhi ya duru kwamba Sheikh Nimr Baqir al Nimr alinyongwa kwa sababu ya hitilafu za kikabila.

Tags