Wahudumu zaidi ya 100 wa kugawa chakula wameuwa Gaza
Idara ya Habari ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina katika Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa zaidi ya wasambazaji 100 wa chakula katika Ukanda wa Gaza wameuawa shahidi katika mashambulizi ya utawala ghasibu wa Israel.
Taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina imesema kuwa, zaidi ya wafanyakazi 100 wanaosambaza misaada ya kibinadamu na wale waliotaka kupokea misaada hiyo katika Ukanda wa Gaza wameuawa shahidi katika kipindi cha wiki moja iliyopita kutokana na mashambulizi ya utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.
Wakati huo huo Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza ongezeko la idadi ya watoto wachanga walio katika hatari ya kufa katika Ukanda wa Gaza kufuatia mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala ghasibu wa Israel na sera za utawala huo za kuzuia kuingia shehena za chakula katika eneo hilo.
Shirika la kimataifa linalofuatilia kiwango cha njaa duniani lililoko chini ya Umoja wa Mataifa pia limeonya katika ripoti yake kwamba ukosefu mkubwa wa chakula katika Ukanda wa Gaza unaosababishwa na mashambulizi ya Israel na mauaji ya kimbari ya utawala huo, umevuka kiwango cha njaa, na iwapo mashambulizi hayo hayatasitishwa na misaada ya chakula kuongezwa, Gaza iitakumwba na hatari ya vifo vya watu wote kwa njaa.