Utawala wa Israel waanzisha mashambulizi mapya Kusini mwa Lebanon
Katika hatua mpya ya chuki, utawala katili wa Israel kwa mara nyingine tena umelenga maeneo ya kusini mwa Lebanon mapema leo Jumatatu kwa mashambulizi makali.
Duru za ndani za harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Lebanon, Hizbullah, zimethibitisha kuwa jeshi la utawala haramu wa Israel limefanya mashambulizi ya mizinga katika vitongoji vya eneo la Naqoura kusini mwa nchi hiyo ya Kiarabu.
Hadi sasa hakuna maelezo yaliyotolewa kuhusu uharibifu uliosababishwa na mashambulizi hayo.
Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imekuwa ikifanya mashambulizi ya mara kwa mara tangu mwanzoni mwa mwezi Oktoba, 2023 dhidi ya vituo vya kijeshi ya utawala ghasibu wa Israel katika kulipiza kisasi hujuma za utawala huo ghasibu dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza na kusini mwa Lebanon.
Utawala wa Israel ulianza vita vyake vya mauaji ya kimbari dhidi ya Ukanda wa Gaza tarehe 7 Oktoba, 2023 baada ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas) kutekeleza operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa ambayo haijawahi kushuhudiwa dhidi ya utawala huo ili kulipiza kisasi kwa ukatili wake uliokithiri dhidi ya watu wa Palestina wasio na ulinzi wala hatia.
Israel imeweka mzingiro kamili katika eneo hilo lenye idadi kubwa ya watu, na kuzuia mafuta, umeme, chakula na maji kwa Wapalestina zaidi ya milioni mbili wanaoishi huko Ukanda wa Gaza.