Idadi ya mashahidi Gaza yakaribia watu 39,000
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i114068-idadi_ya_mashahidi_gaza_yakaribia_watu_39_000
idadi ya mashahidi wa Kipalestina waliouawa tangu kuanza hujuma kinyama ya jeshi la utawala wa Kizayuni huko Gaza (Oktoba 7) imekaribia watuu 39,000.
(last modified 2024-07-14T23:18:04+00:00 )
Jul 14, 2024 23:18 UTC
  • Idadi ya mashahidi Gaza yakaribia watu 39,000

idadi ya mashahidi wa Kipalestina waliouawa tangu kuanza hujuma kinyama ya jeshi la utawala wa Kizayuni huko Gaza (Oktoba 7) imekaribia watuu 39,000.

Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa, hadi sasa Wapalestina 38,584 wameuawa shahidi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, katika kipindi cha masaa 48 pekee Wapalestina zaidi ya 140 wameuawa shahidi na kuifanya idadi ya mashahidi wa Palestina waliouawa katika hujuma ya kinyama ya Israel kufikia 38,584.

Wizara ya Afya ya Palestina imeongeza kuwa, zaidi ya wafanyakazi 300 wa sekta ya afya, vikosi 35 vya ulinzi wa raia na wafanyakazi 135 wa Shirika la Misaada na Ajira kwa Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) wameuawa shahidi katika hujuma inayoendelea ya utawala ghasibu wa Israel.

Tedros Adhanom Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO)

 

Tedros Adhanom Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) amesema: 'Hali ya kiafya ya Ukanda wa Gaza haifai na hakuna mahali palipo salama katika eneo hilo.' Mkurugenzi Mkuu wa WHO ameongeza kuwa Hospitali ya al Maadani haifanyi kazi hivi sasa na ile ya Kamal Adwan na ya Indonesia pia zinakabiliwa na uhaba mkubwa wa mafuta, vitanda vya wagonjwa na vifaa tiba.

Uungaji mkono wa wazi wa Marekani na nchi za Magharibi umepelekea kushuhudiwa faili jeusi la viongozi watenda jinai wa utawala wa Kizayuni wanaoua watu wasio na ulinzi wala hatia. Bila shaka wale wote wanaohami na kuunga mkono jinai za Israel wanahusika pia katika jinai na mauaji ya kimbari ya utawala huo katika Ukanda wa Gaza.