Rais wa Syria atangaza masharti ya kukutana na Rais wa Uturuki
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i114122-rais_wa_syria_atangaza_masharti_ya_kukutana_na_rais_wa_uturuki
Rais Bashar al-Assad wa Syria ametangaza kuwa, yuko tayari kukutana na Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki lakini kwa mashari.
(last modified 2024-07-16T08:04:52+00:00 )
Jul 16, 2024 08:04 UTC
  • Rais wa Syria atangaza masharti ya kukutana na Rais wa Uturuki

Rais Bashar al-Assad wa Syria ametangaza kuwa, yuko tayari kukutana na Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki lakini kwa mashari.

Nitakutana na Erdogan kwa masharti ambayo bila hayo hatutakutana, amesisitiza Rais Bashar al-Assad wa Syria wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari baada ya kupiga kura yake katika uchaguzi wa Bunge.

Rais Assad amethibitisha kuwa Damascus ina mtazamo chanya kuhusu mpango wowote wa kuboresha uhusiano na Uturuki, lakini akaeleza bayana kwamba, atakuna na mwenzake huyo lakini kwa masharti.

Rais wa Syria amesisiitiza kuwa, atakutana na mwenzake wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ikiwa mkutano huo utaleta matokeo ambayo ni kwa maslahi ya nchi zote mbili, ikizingatiwa kuwa tatizo sio katika mkutano lakini katika maudhui yake.

 

Hivi karibuni, Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki alitoa ishara mpya ya kuanzisha tena uhusiano kati yake na serikali ya Syria kwa kutangaza kuwa huenda karibuni hivi akatuma mwaliko kwa Rais Bashar al-Assad wa kutembelea Uturuki.

Katika miaka ya hivi karibuni, na licha ya kupungua mivutano kati ya serikali nyingi za eneo hili na Syria, lakini uhusiano wa Ankara-Damascus haujarudi kama ulivyokuwa zamani. Kwa mtazamo wa serikali ya Syria, kikwazo kikubwa ni uungaji mkono wa Uturuki kwa magenge ya kigaidi yanayofanya mauaji dhidi ya raia na maafisa wa serikali nchini Syria kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi.

Serikali ya Syria imekuwa ikitangaza mara kwa mara kuwa Uturuki inapaswa kukomesha kuzikalia kwa mabavu ardhi ya Syria na kuacha kuunga mkono magenge ya kigaidi. Damascus inasisitiza kuwa "Makubaliano ya Adana" (1998) ndiyo makubaliano bora zaidi ya kutatua masuala yaliyopo kati ya Syria na Uturuki.